Nimesoma maoni yote kila mtu yupo kinyume na maamuzi ya bunge kuhusu ,hukumu ya mpina , kuna siku nilikuuliza kuhusu hili la wengi kukupinga humu hauoni kuwa inaweza kuwa sample ya maoni ya wa tanzania wengi,
Ukasema hizo ni I'd za kujirudia naona pia I'd ya Bantu lady na wengine wote humu ni yangu pia π.
shukran sana kwa kuzingatia na kutilia maanani ushauri,maoni na jibu langu la msingi juu ya dhana ya kuamini na kutegemea complement, constructive and deconstructive criticisms mitandaoni π
kama bado kuna mwanasiasa hajaishi athari ya dhana hiyo basi bado ni learner katika medani hii, ni vizuri akajiandaa kisaikolojia kudhibiti hisia zake wakati wa matokeo, huenda akafanya maamuzi mabaya mno hususani ya kutoa kauli mbovu au mbaya baada ya kuangukia pua kwenye Uchaguzi baada ya kuzingatia na kupumbazwa na sifa za kukubaliwa au kukataliwa mitandaoni π
kuna wagombea na vyama vyao, mpaka tunavyo jadiliana hivi sasa wanateswa na athari za kauli zao baada ya kuvimbishwa kichwa mitandaoni na field ikawa tofauti sana..
na matokeo yake wakaanza kuwabeza na kuwadhihaki wananchi kwa kwaita majina mbalimbali mathalani, ni wajinga, hawajielewi n.k.
wananchi wanakumbuka na bado mtu yule anarudi tena kuomba uongozi kwa aliewaita wajinga. na hivi sasa kuondoa dhihaka hiyo ya kauli kwa wananchi wanaoishi ni ngumu mno na huwez eleweka...
bila shaka nadhani unaweza kua unahisi nazungumzia chama na pengine wanasiasa gani π
kuhitimisha maelezo haya marefu sana, nachelea kusisitiza kwamba mitandaoni na filed mambo ni tofauti kama usiku na mchana π