Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Mimi ningependa Lissu ashinde ingawa simuungi mkono. Sababu zangu ni hizi:
1. Ushindi wake utaondoa dhana ya CDM kuwa ya mtu mmoja ambayo sio kweli
2. Najua Mbowe atakubali matokeo na kumpongeza mshindani wake. Hii itamuongezea yeye na chama chake sifa ya kuwa kweli ni cha kidemokrasia. Aidha, Mbowe ana uwezo wa kuwatuliza wafuasi na kuwashauri nao wakubali matokeo.
3. Kama Wenje atashinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti ajiuzuru mara moja ili kuondoa kiwingu katika uongozi. Heche anaweza kukaimu nafasi hiyo mpaka uchaguzi mwingine utakapofanyika.
4. Lissu amteue mwanamke kuwa Katibu Mkuu wa CDM. Mtu kama CPA Ruge atafaa katika nafasi hiyo. Suzan Kiwanga nae apewe nafasi ya uongozi. Hii italeta balance kidogo ya kijinsia.
5. Manaibu KM waendelee kama ilivyo.
6. Kaimu Mwenyekiti wa Bawacha achaguliwe kuwa Mwenyekiti Kamili wa Bawacha.
7. Mbowe aende nchi za nje akapumzike. Asijihusishe na mambo ya CDM ili isionekane anataka kuongoza kwa remote. Ataweza kuhudhuria vikao vya Kamati Kuu online.
8. Lissu atangaze kufukia yale yote yaliyopita na kuanza safari mpya. Hii itasaidia kuponya vidonda.
9. Lissu aanzishe taratibu za kutambua juhudi zinazofanywa na wanachama wake walio mikoani na wa kawaida. Watu kama Husna wa Chato, Aidan, yule dada aliyewekwa ndani baada ya kujigalagala nje ya ubalozi wa Marekani, Mdude Nyangali na wengine.
10. Aijenge idara ya communication kwa kuweka watu mahiri katika social media n.k.
Amandla...