Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?



Teh teh teh huu uzi unanivunja mbavu.
 
Bora kwny mambo ya kula kuna afadhali kuna kadada kamoja tulienda bagamoyo nikamuuliza unajua kuogelea akasema yupo vzr sn...tumeingia tu kwny pool akapiga vikombe vya maana nusu parapanda ilie mpk akapewa huduma ya kwanza na mtoko ukaishia hapo.
 
Nadhani mnakosea sana kujifanya watu wa hali ya juu sana. Hishima ya mtu ni "Pesa" yake sio uso wake. Nikiingia popote kula au kunywa; Nakula kama ninavyokula pale nyumbani tena nikiwa peke yangu. Nadhani mtanielewa; yaani utadhani hakuna mtu mwingine karibu na mimi.
Wewe ni nani kunichungulia ninavyo kula pesa yangu?? Hivi mnaojidai kuendelea, mwajua kwa nini kukawepo Munu "Menyu??" Yaani kila mtu anunue anachopenda na kulingana na mfuko wake sio ufundi wako wa kujua kula samaki bila kumshika kwa mkono wako.
Ukiingia 5 star hotel na ujuzi wa kula kwa kutumia uma huku mfuko umechanika nadhani utaamkia Segerea na huyo manzi aamkie Sheraton.
Ingia, agiza kuku grilled with spices osha mikono, vunja vunja "karch karch karch"" ukiwa unaangalia sahanini kuwa ni kipande gani kikubwa zaidi ili ukiwahi. Kama hawakuleta sabuni, tumia tissue pangusa mikono. Teremshia na Red wine. Ngojea bill ukiwa unatoboa meno.
Kama yupo aliyekuona mshamba aangalie wallet unapotoa $$$$$. Hapo mshamba ni nani?? Kwani hakikuenda tumboni?? Asikudanganye mtu; Ustaarabu ni Pesa gani unatoqa.
 
Bora kwny mambo ya kula kuna afadhali kuna kadada kamoja tulienda bagamoyo nikamuuliza unajua kuogelea akasema yupo vzr sn...tumeingia tu kwny pool akapiga vikombe vya maana nusu parapanda ilie mpk akapewa huduma ya kwanza na mtoko ukaishia hapo.
Huyo nae ni chikunde teh
 
Sionagi aibu kwenye misosi,nsichokijua nauliza hiki nini? Nyama nashika kwa mkono tena nasema kabisa sorry hivyo visu siviwezi
 
Nachoshukuru mungu sijawahi kuwa na ukaribu na chikunde yoyote yule or mtu anayefake life..kwanza vyakula vya sehemu za hadhi na gharama kubwa sana huwa cjui navionaje havinishibishi alafu hata sio vitamu...madam Evelyn Salt ngoja cku nitakutoa out twende zetu tukale mihogo ya kukaanga or chips nyama choma za vibanda vyetu vya uswahilini πŸ˜‚πŸ˜‚ hope utakuwa comfortable na uta enjoy eeh
 
Nlitaka kumjua mlita post tu!

Ntasoma kesho maana shajua mada ipo jukwaa Lipi.
 
Ewaaaaa ntakua comfortable coooz hayo ndo maeneo yangu (kwa sauti ya chikunde)
 
Dagaa mchele, kachumbali na mlenda pembeni Mkuu hiko chakula kitamu sana aisee.
 
Sijawahi kujivunga aisee na kiukweli sijui kutumia uma na kisu vizuri ila hata huwa sijali.

Mambo ya kuona aibu kwenye kula hapana aisee
 
Mkuu dagaa mchele Na hombo au mchicha wa Nazi ni vitamu asikwambie MTU. Mimi ikifika ijumaa natafuta zile dagaa ili jumamosi nijilie ugali Kwa raha. Jumamosi kula Nyama sijui samaki nakulaga basi tuu ila roho yangu iko Kwa dagaa mchele
 
Hahahahahahaaa.
 
Mbona Bonge LA msosi. Vichwa vya kuku ule Na tembele mbona vitamu Sana. IPO Siku mtaona dagaa Chakula cha watu wa uswahilini mkiendelea hivi
 
Mimi wala sivungi. Nakula Kwa mkono Kwa raha zangu. Mambo ya kuigjza unakula hushibi haihusu. Sana Sana nikiona haya ntakula zangu chips Na firigisi au mishkaki ya samaki najua hamna mbwembwe za kisu. Ila kuku Na samaki nakula Na mkono wala sioni aibu. Tumbo langu mwenyewe aibu ya kazi gani sasa. Unakuta MTU anakula Kwa kisu anahangaika. Nawaambiaga embu nawa mikono uenjoy Chakula hakijaletwa bure hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…