Unafahamu kuwa Google imerekodi kila safari yako bila wewe kujua?

Unafahamu kuwa Google imerekodi kila safari yako bila wewe kujua?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Google imerekodi kila safari yako ya kwenda hospitali mwaka huu, na hata mizunguko yako ya usiku wa manane. Simu yako inatuma taarifa (updates) zako kila baada ya sekunde 96. Simu za Android zinatuma taarifa zako mara 20 zaidi kwenda Google ukilinganisha na jinsi iPhone inavyotuma kwenda Apple.

Kila sehemu unayoenda na simu yako, kila mtaa, kila kituo. Saa 24, hata ukiwa umelala. Mahakama iliwahi kuipiga Google faini ya Dola za Kimarekani Milioni 425. Watu walizima (turn off) mfumo wa kufuatiliwa, lakini Google iliendelea kuwafuatilia kimyakimya, na wakajikuta wanalipa tena faini nyingine ya Dola Milioni 391 kwa mawakili wa serikali 40 kutokana na kosa hilohilo.

Siri ni kwamba, Google ina mifumo miwili tofauti ya kufuatilia watu: mmoja unaitwa Web and App Activity na mwingine unaitwa Timeline. Kuzima mfumo mmoja hakuzimi wa pili. Google walitengeneza hii mifumo hivi makusudi.

Hivi ndivyo unavyoweza kuzima:

📱 Kwa Watumiaji wa iPhone:
Fungua App ya Google Maps, gusa picha yako ya profile kule juu kulia, chagua "Your Timeline" > "Settings and Privacy". Gusa "Location History" kisha izime (turn it off). Hakikisha pia unafuta (Delete) historia yako yote ya mahali ulipokwenda.

📱 Kwa Watumiaji wa Android: Ingia kwenye "Settings" za simu yako. Gusa "Google" > "Manage your Google Account" > "Data & privacy". Gusa "Timeline" na uizime. Kisha rudi nyuma na uzime pia "Web & App Activity". Unatakiwa kuzima vyote viwili.

Simu yako inajua kabisa kwamba Alhamisi iliyopita ulienda kumuona daktari 🫣

Inajua uliketi kwenye maegesho ya magari (parking) kwa dakika 9 kabla ya kuingia ndani. Inajua ulikuwepo hapo kwa dakika 47. Na inajua kabisa wakati unarudi nyumbani ulipitia duka la dawa.

Na Google imehifadhi (save) haya YOTE. Kila kituo. Kila ulipokwepuka njia. Kila "mzunguko mfupi" ulioufanya saa tano usiku 😳

Hizi sio stori za vijiweni au nadharia za kufikirika. Nenda kaangalie sasa hivi. Ingia kwenye Google Maps > Gusa picha yako ya profile > Your Timeline.

Shuka chini uangalie (scroll). Utashangaa na tumbo litakata!

Kila safari ya kwenda hospitali. Kila mizunguko yako ya usiku wa manane. Kila sehemu uliyowahi kumwambia mtu "sijawahi kufika." Yote yapo pale kwenye ramani, yakionyesha mpaka muda na saa 📍​
 
Kila sehemu unayoenda na simu yako, kila mtaa, kila kituo. Saa 24, hata ukiwa umelala
Mkuu,
Kama hao Google wanahifadhi taarifa za kila mwenye Android na mwenye iPhone kwenye kanzi data zao, ina maana wana mzigo mkubwa mno wa data maana ni za billions of people!
Wanazitumiaje na kwa manufaa gani?
 
Google ilitengenezwa na ma CIA kwa ajiri ya kukusanya data ulimwengun pote.

ile ni injini ya mitandao yote ila kila unacho google kuuliza/kutafta data zinakusanywa kule
 
Mkuu,
Kama hao Google wanahifadhi taarifa za kila mwenye Android na mwenye iPhone kwenye kanzi data zao, ina maana wana mzigo mkubwa mno wa data maana ni za billions of people!
Wanazitumiaje na kwa manufaa gani?
Google imeundwa nyuma ya CIA.
 
Watakusanya data za pascal mayala sisi wengine hakuna maandish au majina ya kwel tunayoweka humu email tu ninazo 8 na zote ni feka nida ni fake lesen za udereva majina fake so google mi hamuwez nichunguza
 
Iyo mifumo haina athari kwa uku bongo land maana wengi tunaomiliki izo simu hatuna athari kwenye makampun wala maofisi maybe tufuatiliwe na wale wanaofanya dolia mtandaon
 
Back
Top Bottom