JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Upasuaji wa kwanza wa Uzazi (C-Section) ulifanikiwa kufanyika Barani Afrika, ambapo Mama na Mtoto wote walikuwa salama, mara nyingi ujuzi huu, ingawa Daktari Mwingereza, James Barry amekuwa akihusishwa zaidi na upasuaji huu kutokea Cape Town, Afrika Kusini.
Caesarian Section (C-Section) ni upasuaji wa uzazi unaofanyika kwa mama Mjamzito kama mbadala pale Mama anaposhindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
Inasemekana Wabanyole, kabila kutoka Uganda, zamani wakijulikana kama Bunyoro ndo Watu wa kwanza kufanikiwa kufanya upasuaji huo bila kuhatarisha Maisha ya mama na Mtoto, ukilinganisha na nchi za Ulaya ambako walilenga kuokoa Maisha ya Mtoto peke yake enzi hizo.