Unafanyaje kama mkeo ni mbea kupitiliza?

Unafanyaje kama mkeo ni mbea kupitiliza?

Au waifu mwenyewe anaweza kubanwa sana na umbea, akaupeleka mwenyewe Ubalozini kwa miguu... Waifu wa aina hiyo ni noma sana...
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] anakufungisha, kwanza unawezaje kuwa na type hiyo aisee
 
Nilikuwa na ke wa aina hiyo, mpaka kero kila kitu utakachofanya anatoa siri zote za ndani, hata kama unadili la kupata hella kibaya zaidi ukiwa haupo home anakufanyia upekuzi na kusoma documents na mpaka kupeleka kwa jirani kuwaonyesha tuna hiki
mm sikurijua hilo maana mm ni mtu mkimya sana( introvent) nilikuja kuambiwa na jirani mambo yote anayowasimuliaga mambo yote ya ndani mpaka aibu
 
Kazi unayo.Kaa naye umueleze anavyokukwaza,kukuanika,kuhatarisha familia na kukuaibisha kwa majirani.

Anayoyafanya ni tabia mbaya kabisa.Atakukosesha hata majirani wa kuongea nao.Anza kwa kuongea naye.
Unajua kumkalisha mtu mzima na kumuonya mambo ya kitoto hii kitu inahitaji uwe na kipaji maalum [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Sasa najiuliza nimfanyaje nilishamuonya tukaishia kugombana si mara moja. Ukimwambia anakataa na hasa kulia mwisho tunagombana!

Je, wewe unafanyaje kama una mke wa hivi ndani?

Naomba mnisaidie kushauri

KENZY tafadhali msaidie
 
Back
Top Bottom