Unafanyaje kama mkeo ni mbea kupitiliza?

Unafanyaje kama mkeo ni mbea kupitiliza?

Mr Chromium

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2020
Posts
2,761
Reaction score
3,835
Hello Jf

Natumaini mtasoma na kunipa ushauri kulingana na uzoefu wenu au maarifa kadili ya busara zenu. Nimeoa ninaishi na mke na nina mtoto mmoja!! Kifupi mimi ni mtu busy sana sishindi sana nyumbani na hata nikishinda sijuani sana na majirani

Sasa kati ya majirani nilio nao kuna jiran mmoja tupo nae karibu sana n mmama mtu mzima umri wa mama yangu!! Na mazoea yametokana na ukaribu na utegemezi nilio uweka wakt nanunua eneo hili naloishi hapa mtaani kwani ilinibidi niwe nawasiliana nae mara kwa mara kupata taarifa saahihi juu ya mmiliki wa mwanzo, migogoro ya eneo nk

Sasa amekua akiniita na kunishauri vitu mbalimbali!!Ikiwa pamoja na maneno yanayosikika mtaani. Kifupi chanzo n mke wangu n mmbea sanaa!! kwa kifupi hana siri hata mojaaa!! Kila kitu anasimulia kwa watu na majirani !!Yaan namaanisha kila kitu, hata vitu vya siri. Ni mtu wa kujikweza na kuropoka yaan hiyo taabia ndiyo inayosababisha aongee vitu bila kuulizwa

Ingawa sijazoeana na watu mtaani ila kila mtu anajua kwangu kukoje kuna nn, na viwanja wapi, nyumba wapi, Tunakula nini, nafanya kazi wapi, nimesafiri, nimerudi, yaan kila kitu, nimemfanya leo au sijamfanya,nina boxa ngap nk

Nikimaanisha kila kitu eleweni achilia mbali umbea wa wanawake ule wa kawaida ambao kila mwanamke anao, naongelea mdomo, majigambo n umbea wa kutoa kila na vyote vya ndan na nje. Tabia nyingine zinavumilika lakini hii naona inanikera

Nimekua nikisikia minong’ono kadhaa,mengine nakuta story sasa huyu mama jiran ndo atleast anakifua kuniambia baadhi ya mambo lakini wengine wananichora tu, kuna vitu majiran wanavijua mimi sivijui

Sasa najiuliza nimfanyaje nilishamuonya tukaishia kugombana si mara moja. Ukimwambia anakataa na hasa kulia mwisho tunagombana!

Je, wewe unafanyaje kama una mke wa hivi ndani?

Naomba mnisaidie kushauri
 
🤣🤣🤣🤣🤣, kwanza pole kwa yaliyokukuta. Yaan unataka kusema mkeo frdge lake haligandishi, pole sana.


Kama n mama wa nyumban mtafutie kaz ya kufanya, itakayomuweka bize mnooo atapunguza umbea kwa kias kikubwa sana kama s nusu bas nusu na robo ya umbea atapunguza.
 
Umbea kwa Ke yeyote ni sawa na mate na ulimi isipokuwa kuna umbea mzuri na umbea mbaya.

Ikiwa kwa siku 1 Ke anaongea maneno zaidi ya 500 tofauti na Me ataongea maneno 200, unadhani muda wote huo atakuwa anaongea ukweli tu bila ya umbea?
 
Hello Jf
Natumaini mtasoma na kunipa ushauri kulingana na uzoefu wenu au maarifa kadili ya busara zenu!!..

Nimeoa ninaishi na mke na nina mtoto mmoja!!
Kifupi mimi ni mtu busy sana sishindi sana nyumbani na hata nikishinda sijuani sana na majirani !!

Sasa kati ya majirani nilio nao kuna jiran mmoja tupo nae karibu sana n mmama mtu mzima umri wa mama yangu!! Na mazoea yametokana na ukaribu na utegemezi nilio uweka wakt nanunua eneo hili naloishi hapa mtaani kwani ilinibidi niwe nawasiliana nae mara kwa mara kupata taarifa saahihi juu ya mmiliki wa mwanzo, migogoro ya eneo nk!

Sasa amekua akiniita na kunishauri vitu mbalimbali!!Ikiwa pamoja na maneno yanayosikika mtaani!!

kifupi chanzo n mke wangu n mmbea sanaa!! kwa kifupi hana siri hata mojaaa!! Kila kitu anasimulia kwa watu na majirani !!Yaan namaanisha kila kitu ,, hata vitu vya siri !!!… Ni mtu wa kujikweza na kuropoka yaan hiyo taabia ndiyo inayosababisha aongee vitu bila kuulizwa!!

Ingawa sijazoeana na watu mtaani ila kila mtu anajua kwangu kukoje kuna nn, na viwanja wapi,nyumba wapi,Tunakula nn, nafanya kazi wapi,nimesafiri,nimerudi, yaan kila kitu ,nimemfanya leo au sijamfanya,nina boxa ngap nk

Nikimaanisha kila kitu eleweni…achilia mbali umbea wa wanawake ule wa kawaida ambao kila mwanamke anao!!..naongelea mdomo,majigambo n umbea wa kutoa kila na vyote vya ndan na nje!
Tabia nyingine zinavumilika lakini hii naona inanikera

Nimekua nikisikia minong’ono kadhaa,mengine nakuta story sasa huyu mama jiran ndo atleast anakifua kuniambia baadhi ya mambo !!… lakini wengine wananichora tu,,,, kuna vitu majiran wanavijua mimi sivijui

Sasa najiuliza nimfanyaje nilishamuonya tukaishia kugombana si mara moja!!…
Ukimwambia anakataa na hasa kulia!!..mwisho tunagombana!!

Je ww unafanyaje kama una mke wa hivi ndani???

Naomba mnisaidie kushauri!!

Aisee pole sana nahisi unavyoteseka. Maana familia nyingi siku zote zinahitaji usiri.Nadhani pia ni umri na elimu yake vitakuwa ni vya chini labda.Kwamba akikua atabadilika.sema kwa sasa kama itakufaa,ili kuepusha kuhujumiwa, jiwekee siri mwenyewe kwanza.

Kwa ajili ya dharura unaweza chagua watu wako wa karibu uwe unawajulisha unakwenda wapi au una projects gani na wapi.Ili ikitokea unadondoka ghafla kuna wa kufuatilia issues zako.

Lakini wakati mwingine inawezekana unasababisha hayo yote, yaani anakosa muda wa kuwa nawe ili akusimulie vitu.maana anaonekana ni mke anayependa sana attention.Yaani apate mtu wa kumsikiliza
 
Kazi unayo.Kaa naye umueleze anavyokukwaza,kukuanika,kuhatarisha familia na kukuaibisha kwa majirani.Anayoyafanya ni tabia mbaya kabisa.Atakukosesha hata majirani wa kuongea nao.Anza kwa kuongea naye.

Nimeongea nae sana !! shida ye anapenda kujikweza nakujikuta anaongea kila kitu kwa kila mtu
 
Mimi nilikuwa na mwanamke wa dizaini hiyo habar zangu utazikuta kwa mdogo wangu mara mama yangu nikafanya utaratibu kidogo nikamwambia sitaki habari zako tunaongea kitu unawapelekea ndugu zangu baada ya hapo aliona kila nalo fanya simshirikishi kabisa mbona alikuja ananiomba samahani..

nikamwambia utaratibu ni huo mama kwasababu unaweza ukasema neno hata kwa adui zangu hata nikauawa au dili ikafeli sasa wewe baki na mdomo wako.
 
Technique ya kwanza umeshapewa kumkeep busy by anyway sio biashara tu yaan kuna ile unamkeep busy mpaka akirudi nyumbani hata ham hana kuhusu kupiga umbea kwenye kazi utakayomtaftia hakikisha kazi unayomtaftia aimpi muda wa kupga umbea eg kuna kazi unaweza ukawa unafanya inakuitaj kuwa active all over the time unakuta kama mteja hayupo unahitajika kupanga bidhaa Mara kuwasiliana ili kupata mzigo mpya Mara kudocument mauzo nk Mimi nakupa kama example utaongeza na zako katika kuidisign hyo kaz kuringana na mazingira uliyopo njia ya pili ukiona mwenzio hagandishi mipango na info sensitive tunza mwenyewe
 
Back
Top Bottom