Unafanyaje kuishi maisha ya kigeto geto bila kupika?

Unaweza kupika wali nyama, maharage na mboga za majani pembeni na vidagaa vya kutia hamasa pembeni kwa 2000?
Haujawahi kula kwa gharama hii! Hata robo ya nyama mpaka iive siyo elf 2, na sikuizi wengine hawapimi ΒΌ ya nyama ni kanzia Β½ nakuendelea
 
Fanya kama mimi. Nachemsha nyama, nakaanga dagaa na samaki. Naweka kwenye friji. Maharage nikitaka nanunua ya kuchemsha yanapimwa kwa mamantilie. Sasa wewe eti ukitaka kula nyama ndio unanunua buchani hapo lazima uumie.

Nina viungo kama mdalasini, hiriki na tangawizi na maziwa ya kopo. Nachemsha chai nikitaka.

Nanunua nyanya na vitunguu na mara chache nanunua viazi vitamu au magimbi ila mihogo huwa siipendi. Napata vitafunwa. Unga, mchele, mayai, ngano visikose.

Napika sio sababu nishibe mimi hula chakula kidogo tu. Napika sababu ni mbaguzi mkubwa wa vyakula na mapishi, siwezi kama wewe hapo kula popote ninapokuta mgahawa. Pia quality na style kwamba nikimiss kitu fulani nipike au nipikiwe. Mfano huwa natamani 'supu' ya karanga za kusaga, sasa mamantilie gani akupikie hivyo si anakucheka.
 
Kupika Inategemea na mood na ratiba zitakavyokua mfano mwezi wa tano nilipika sana,cost za kununua mazaga zaga zilifika %45 ya budget kwa mwezi wa tano [emoji116]



Ila mwezi huu wa sita ulioisha sikuwa kabisa na mzuka wa kupika nilikua napika kwa manati na cost za hayo mazaga zaga zilishuka hadi %15.9



Nasubiri nione huu mwezi wa saba utakavyokua upande wa maskolodinyo
 
Ukipika mwenyewe siyo kwamba gharama inapungua hata uwe unakula vitu basic tu ila kama wengine walivyosema kwa kiasi kikubwa utakuwa unakula vyakula fresh. Huko migahawani mazingira siyo safi na wapikaji siyo wasafi ni kwamba huwa tunafumba macho tu vyakula vipite kwenye koo.

Kuhusu kuosha vyombo, anza kuosha wakati unapika. Chakula kikiiva hakikisha vyombo vyote ulivyotumia kupika tayari ni safi inakupunguzia mzigo baadae. Ukimaliza kula utajikuja umebaki kuosha vitu vichache sana ulivyotumia kama sahani, vijiko na vikombe. Osha hivyo fasta kabla uvivu haujakuingia.
 
Hesabu kali sana hizi πŸ˜‚πŸ˜‚ umenishinda πŸ™Œ
 
Pika mwenyewe unakula kitu moyo unashangiliaa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sawa ila mpaka ule moyo unashangilia, kumbuka hapo lazima itumie si chini ya bajeti ya mboga 8,000 na zaidi hapo utakuwa umeokoa matumizi au umeongeza tumizi
 
Sahihi 🀝🀝
 
Wee endelea na hayo maisha mzeya. Mambo ya kupika pika ni ya kike.
Kwanza unapoteza muda tuu. Wee lengo lako sii tumbo lishibe.
Hamna kitu kinakera kama kuosha vyombo
 
Ni wazo zuri sema muda wa kununua fridge/ freezer ndio sina maana naishi kama ndege kesho mkoa huu mwezi ujao wilaya ile hapo utanunua vitu kweli labda ununue vitu hivi ukiwa umesimika kambi kabisa sehemu moja
 
Wee endelea na hayo maisha mzeya. Mambo ya kupika pika ni ya kike.
Kwanza unapoteza muda tuu. Wee lengo lako sii tumbo lishibe.
Hamna kitu kinakera kama kuosha vyombo
Kumbr tuko wengi aisee nikajua niko peke yangu kuhusu hili suala πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mama ntilie yuko blid akajikuna kunako akaedelea kukatakata kachumbari,mtoto kajisaidia akamtawaza kwenye beseni lakukandia maandazi,ukinikuta kwa mama ntilie niite mbwa
Hata nyumbani hili unalosema linaweza kufanywa na mkeo au mfanyakazi wako, kikubwa uwe mzima tu basi mengine hayo ni matokeo.

Kuna wanawake wachafu ajabu yaani unaona kabisa hapa hamna kitu kupika, hata ndani ni holela sema kama ukiangukia kwenye mtego huu omba isiwe utajuta. Ukitaka kuja na mgeni mpaka utangulie kwanza ukahakiki kama mazingira ni salama ndio umpokee mgeni uliyepanga kuja nae kwa pamoja
 
Kigezo changu cha kwanza kwa wife material ni mwanamke msafi,kinyume chake hafai kuweka ndani
 
We hakikisha una sufuria zako 2 tu.
Moja ya mboga moja ya ugali. Ukinaliza kupika unakula humo humo.
Kwaio ukitaka kupika tena lazma uyaoshe. Automatically unakua umeondoa jam ya kuosha vyombo.
Sufuria la ugali ndo litatumika kuchemsha hadi chai. Unaacha ipoe unainywa from sufuria kistaarabu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…