Unafiki na Ukweli wa Posho Bunge Jipya la Katiba Sisi ni Wanafiki Mno!!

Unafiki na Ukweli wa Posho Bunge Jipya la Katiba Sisi ni Wanafiki Mno!!

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,400
[h=3][/h]

- Ukweli ni kwamba Serikali inahitaji kujiangalia upya na haya mambo kwa sababu hayatokei kwa bahati mbaya, kwa nini wananchi wanalilia posho kubwa ni kwa sababu wameona pesa za umma zinatumika hovyo hovyo bila melezo na wao sasa wanataka kuzitumia pia, I mean Tume imetumia Billioni 70 kutengeneza Rasimu, halafu zimetumika Bilioni 8.2 kukarabati Bunge kwa ajili ya kukaa chini kwa siku 70 tu, sasa kwa msururu huo wa matumizi ya ajabu namna hiyo unategmea nini kutoka kwa wananchi wa bunge la katiba si na wao wanataka kuchota laki saba kwa siku, yes kama wajumbe wa Rasimu walikuwa wanachota 647,000 kwa siku kwa nini na wao wasichote pia?

- I mean juzi usiku nikiwa Dodoma nilikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mahesabu kwa masaa mengi nikaamuliza hizi pesa zote zimetokea wapi na ziliidhinishwa na nani matumizi yake hata yeye hakuwa na jibu la uhakika, sasa hili Taifa tunategemea nini hasa? Na huwezi kuwa na akili timamu ukasema ni kosa la Rais sasa tunataka Rais afanye kazi za Kamati ya bunge ya mahesabu?

-So nimeamua kuikata kata hii ishu vipande vipande kwenye makala yangu ya kila Jumapili kesho kwenye Gazeti la Jambo Leo.

Le Mutuz
 
Kiranja mkuu ndio tatizo kubwa!

Huwezi kubariki uhujumu uchumi kwa kigezo cha kushauriwa!
 
Umeongea jambo zuri sana ila Rais wetu abaki kundini katika kurekebisha hii hali,unamtoaje wakati yeye ndio number one executive?????!!!!!

Muache mzee kundini sababu kauli yake tu inatosha kumaliza hili lakini pia hao wajumbe kawaidhinisha yeye so analo la kuwaambia! !!!!!!!

"Vinyago vya kuchonga mchana usiku vinamtishia mchongaji"
 
Hii nchi kumbe kuna pesa za kumwaga ..
Hiv waalimu wanaodai pesa zao wanajisikiaje kuona mtu anapokea laki 6 kwa siku.

Mi nawalaumu waalimu na wananchi wapo wapo tu. Wakat wengine wana ( Chukua Chakwako Mapema "CCM" )
 
Ndiyo maana watu tunasema CCM hawafai kuongoza Nchi . Ni shida ya watu uwa waizi na mafisadi . CCM yako sasa unalia lia nini ? Lazima wahongwe waharibu mchakato wa Katiba uwalinde kuendelea kuiba . Mimi nashangaa sana mnasepa CCM inawatetea wanyonge . Kivipi ina watetea ?
 
Umeongea jambo zuri sana ila Rais wetu abaki kundini katika kurekebisha hii hali,unamtoaje wakati yeye ndio number one executive?????!!!!!

Muache mzee kundini sababu kauli yake tu inatosha kumaliza hili lakini pia hao wajumbe kawaidhinisha yeye so analo la kuwaambia! !!!!!!!

"Vinyago vya kuchonga mchana usiku vinamtishia mchongaji"

- Salute!!

Le Mutuz
 
Ndiyo maana watu tunasema CCM hawafai kuongoza Nchi . Ni shida ya watu uwa waizi na mafisadi . CCM yako sasa unalia lia nini ? Lazima wahongwe waharibu mchakato wa Katiba uwalinde kuendelea kuiba . Mimi nashangaa sana mnasepa CCM inawatetea wanyonge . Kivipi ina watetea ?

Huko wapo wote taja rangi ,majina ,mavazi na hata alama.za vidole wote kundi moja hakuna wa mchuzi wala kulumagia!!!!!
 
Nani ndiye wa mwisho kuidhinisha? Ina maana hizo kamati zikishaamua basi fedha zinatoka bila kiranja mkuu kusign ?

Mbona kipindi kile cha Mgaya na TUCTA Kiranja Mkuu alisema NO? Hizi zimemshinda nini?
 
Ndiyo maana watu tunasema CCM hawafai kuongoza Nchi . Ni shida ya watu uwa waizi na mafisadi . CCM yako sasa unalia lia nini ? Lazima wahongwe waharibu mchakato wa Katiba uwalinde kuendelea kuiba . Mimi nashangaa sana mnasepa CCM inawatetea wanyonge . Kivipi ina watetea ?

- Wajumbe wa Kamati ya Mahesabu ya bunge ndio wahusika wa hili 100% na sio wote ni CCM kaka!!

Le Mutuz
 
Nani ndiye wa mwisho kuidhinisha? Ina maana hizo kamati zikishaamua basi fedha zinatoka bila kiranja mkuu kusign ?

Mbona kipindi kile cha Mgaya na TUCTA Kiranja Mkuu alisema NO? Hizi zimemshinda nini?

- Kaka hii kamati ilipokataa mkataba wa Buzwagi Rais alifanya nini alipigana nao?

Le Mutuz
 
Safi sana. Kwenye hiyo nakala gusia pia suala la wale wezi walioiba pesa ya epa na kuombwa na mkulu wazirudishe ili awasamehe,na ikawa hivyo.
 
Nakuunga Mkono Le Mutus.Tshs.300,000/= ni nyingi na Wajumbe wanaelewa hili.Wabunge wa Bunge la Katiba Kimsingi wanaona kama wamedhalilishwa kwa kulipwa Kiasi Kidogo kuliko Wajumbe wa Tume ya Warioba.Wanajua Pesa za Tanzania hazina Usimamizi na zinafujwa na Mamlaka husika kupitia Semina,Safari,Warsha,Makongamano na Posho.Sioni Mantiki ya kumtoa Mwenyekiti wa CCM kwenye Ufujaji huu wa Fedha za Watanzania.
Pangekuwa na Mwenyekiti wa CCM(Rais) makini kama Mwl.Nyerere,Sidhani kama kuna mtu angefungua Mdomo kusema wanayotamka sasa.
 
- Kaka hii kamati ilipokataa mkataba wa Buzwagi Rais alifanya nini alipigana nao?

Le Mutuz
Nchi hii inaongozwa na CCM ndugu yangu.Wananchi walimchagua Kikwete na CCM iwaongoze.Kamati ikipendekeza Ujinga na Rais akikubali tutamlaumu Rais maana ndie tuliyemchagua.Lakini mwisho wa yote tutajilaumu Wananchi wenyewe kwa kutochagua Kiongozi Bora.
 
- Yaani Rais ashuke chini mpaka kwenye haya mambo na wakati Kamati ya Bunge ipo? Haiwezekani!!

Le Mutuz
Kama anashuka chini kuwateua wakuu wa wilaya na wa mashirika ya umma anashindwa nini kuingilia kati ubadhilifu wa mabilioni ya walalahoi.
Kwa nafasi aliyonayo haya anayajua nakuyabaliki kabla hayajaamuliwa.
 
- Yaani Rais ashuke chini mpaka kwenye haya mambo na wakati Kamati ya Bunge ipo? Haiwezekani!!

Le Mutuz

Kinadharia unaweza kuwa sahihi; hata hivyo yaliyotokea yametokea, vyombo tulivyotegemewa viwe makini kulinda rasilimali za umma kwa faida ya walio wengi ndio hivyo vimekumbwa na ubinafsi wa kutisha kwa faida ya mafisadi wachache. Now, Mh. Rais kama Kiongozi Mkuu, in his capacity, amechukua hatua gani? Au hapaswi?

Nadhani tungependa kuona msimamo wa Rais kwenye hili na sio kukaa kimya kwa kigezo kwamba kuna vyombo vinavyopaswa kutimiza majukumu yake au eti Rais hawezi kufanya kila kitu. Wakati mwingine Rais anapaswa kuwa bold, clear, and straight to the point badala ya kuzungukazunguka kupitia media au "wasemaji" wake.

Rais na aseme sasa tumsikie.
 
- Yaani Rais ashuke chini mpaka kwenye haya mambo na wakati Kamati ya Bunge ipo? Haiwezekani!!

Le Mutuz

Mkuu unaposema kamati ya Bunge ipo naona unakosea. Kamati ya Bunge kazi yake ni oversight na kazi hii ya oversight mara nyingi huwa ni postmortem yaani hufanyika baada ya matumizi kufanyika na siyo kupitisha matumizi. Hivyo basi hata kama hayo matumizi yametumika nje ya taratibu itafika wakati ambapo Kamati itahoji na siyo kuhoji kabla ya matumizi. Hii itakuwa ngumu kwa sababu sasa Bunge litakuwa kama linaingilia utendaji wa mhimili mwingine wa dola. Hapa kama kuna shida hizo ulizozisema basi kinachotakiwa kusakamwa ni muhimili wa serikali (executive). Kama unamuondoa Rais ambaye ndiye mkuu wa serikali (ni kweli hawezi kusimamia kila kitu) sawa, lakini kuna watu ambao amewapa mamlaka ya kusimamia vitu hivi hivyo hao ndio wa kulaumiwa kama mambo yanaenda kombo na si kamati ya Bunge.
 
Back
Top Bottom