Unafiki na Ukweli wa Posho Bunge Jipya la Katiba Sisi ni Wanafiki Mno!!

Unafiki na Ukweli wa Posho Bunge Jipya la Katiba Sisi ni Wanafiki Mno!!

- Wajumbe wa Kamati ya Mahesabu ya bunge ndio wahusika wa hili 100% na sio wote ni CCM kaka!!

Le Mutuz

kaka kuna saa unaongea pumba tu

na exposure yote ya kukaa marekani siamini unaandika hiki

kwa kukusaidia tu matumizi ya serikali ya tanzania huanzia huko huko serikalini....na kwa uhuni wa serikali ya awamu ya nne (sina uhakika na awamu nyingine), kuna matumizi mengi sana ambayo hayana utaratibu ndio maana unakuta kamati haina taarifa wala meno ya kudhibiti.....hivi hata hupanui ubongo wako kujiuliza kuna pesa kiasi gani kimetumika nje ya budget awamu hii ya nne huku budget husika ikiwa na.upungufu wa hela maeneo mengi?
 
- ulipoanza na maneno ya ukali na ya mtaani nilidhani una hoja kumbe ni pumba unazozisema mwenyewe, nakuuliza swali kwenye mkataba wa Buzwagi ilikuwaje ulianzia Serikalini au Ulianzia kwenye Kamati ya bunge? Tumia akili kidogo tu kaka ni uzembe wa Viongozi wetu kutojua mamlaka zao ndio maana siku zote wanaamuliwa na wasiohusika hakuna pesa yoyote ya Serikali inayotakiwa kutumika bila ruhusa na Kamati ya bunge ya mahesabu,

- Sasa imagine hiyo kamati ina watu kama wewe ndio hasara kwa Taifa, next time fanya utafiti kabla hujaongea maana umeongea pumba tupu kaka!!

Le Mutuz
 
Nadhani akili yako ni kutaka kuonyesha kwamba hata wapinzani wameshiriki. Kamati ni kama auditor anakagua baada ya matumizi hivyo usitake kutuona wote hatujaenda shule. Kosa ni la Serikali yetu hapa namaanisha Rais Kikwete & PM Pinda.
 
- Kaka hela ni lazima ziwe allocated na Kamati kwanza toka hela zikatumika kwanza ndio wakaja kuelezea kamati, ndio maana mabishano hayaishi humu maana siku zote kuna watu kama wewe wanaojifanya wanajua kumbe ni zero tupu!!

- ni Dunia ya wapi kaka uliwahi kusikia Serikali inatumia pesa kwanza halafu ndio inaenda bungeni kuomba bajeti, please kaka mbona ni kutumia akili kidogo sana tu!!

Le Mutuz
 
Jamani wana janvi wenzangu, hivi ni kwanini katika suala la posho ccm na wapinzani huwa wamoja? Au pesa mwanaharamu? Zitto kabwe aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba alikataa posho za bunge( sitting allowances) sikusikia mpinzani mwingine yeyote alie ungana nae kutete posho zifutwe. Hasa kutoka chama chake ambacho ndicho kinaongoza upinzani bungeni. Juzi kati limekuja suala la wajumbe wa baraza la katiba kujadili posho kwamba ni kidogo(300,000) kwa siku. Wapinzani waliona ni sawa tena baadhi wanatetea iongezwe zaidi ya hiyo. Hii imenijengea taswira kwamba upinzani upo kama danganya toto tu katika nchi hii wote ni wachumia tumbo; wananchi wasidanganyike kwamba kuna watu wanawatetea! Wajipange kisaikolojia kupambana na maadui wa tatu wa binadamu.
 
Wanazikana kwenye media na mitandao ya kijamii huku kwenye account zinaingia!

Hii ndio Tanzania yetu aliotuachia Nyerere!
 
Kaka acha kupotosha budget inapitishwa bungeni lakini Wanavusha matumizi nani anachukuliwa hatua. Je hata report za CAG husomi nani kawajibishwa hapo kamati inahusika vipi?
hacha utani na watu bana.
 
Ndiyo maana watu tunasema CCM hawafai kuongoza Nchi . Ni shida ya watu uwa waizi na mafisadi . CCM yako sasa unalia lia nini ? Lazima wahongwe waharibu mchakato wa Katiba uwalinde kuendelea kuiba . Mimi nashangaa sana mnasepa CCM inawatetea wanyonge . Kivipi ina watetea ?

Acha kuingiza itikadi za Vyama watu wanapo simama kama waTanzania, Mbowe ni mjumbe wa Kamati ya Kudai Posho na alipochaguliwa Makofi yalirindima ukumbini tofauti na Lukuvi walimzomea kwa kuwa walijua atakwamisha juhudi za kujiongezea Posho, Kwenye hili la Posho Richard Ndassa, Nassari, Lema,Komba nk walikuwa kitu kimoja bila ya kujali vyama walivyotoka, Kama unachagua wa kukosoa kwa kuangali vyama utakuwa ni Adui wa Taifa kuliko hao wanaodai posho.
 
Kuna wapinzani wachache wako kizalendo kuhusu hizo posho. wapo waliojitokeza kupinga kuongezwa kwake lakini wengi wao wamekaa kimya kutoonesha misimamo yao. binafsi natafsiri wote waliokaa kimya wanataka waongezewe.
 
Unaonekana kufumbuka macho, na mchango wako huenda ukawa na manufaa kwa jamii,kama hayo unayoyasema yanatokana na dhamira ya kweli.
Tahadhari ukiwa unaendelea na makala zako,usijaribu kumtoa Sammy kwenye sakati hili,huyo ndiye mwenye kauli ya mwisho,kama haoni pa kurekebisha hiyo itakuwa ni mojawapo ya sifa yake ya udhaifu. Hakuna mtu anaweza kuingia ktk anga zako na akajiamulia kufanya atakavyo isipokuwa kwa kibali toka kwako. Vinginevyo watendaji watakuwa wameshamsoma vizuri na wanaelewa jinsi ya kudeal na udhaifu wake. Hii kwa lugha rahisi ni kuwa walishamdharau to the maximum.
Leo umeonyesha tofauti kubwa sana na Lukosi,na haya ndiyo tunayoyatarajia kwenu wasomi kwa manufaa ya kujenga taifa letu bila ku-base kwenye itikadi za vyama.
Nadhani wengi watakuwa wameshtushwa na huu mchango wako wa leo.(I am happy for you).Ila kabla sijakumwagia sifa nyingi ngoja niendelee kuzifuatilia makala zako maana sometimes mko very unpredictable.
Ponya taifa letu na ujitenge na uwendawazimu wa Lukosi. Big up for today.
 
Ubinafsi umekua na kuonekana bila aibu kuwa ndio namna ya kuishi. Uzalendo na kutumikia umma imebaki katika historia. Hili ni tatizo la kitaifa.
 
Jamani wana janvi wenzangu, hivi ni kwanini katika suala la posho ccm na wapinzani huwa wamoja? Au pesa mwanaharamu? Zitto kabwe aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba alikataa posho za bunge( sitting allowances) sikusikia mpinzani mwingine yeyote alie ungana nae kutete posho zifutwe. Hasa kutoka chama chake ambacho ndicho kinaongoza upinzani bungeni. Juzi kati limekuja suala la wajumbe wa baraza la katiba kujadili posho kwamba ni kidogo(300,000) kwa siku. Wapinzani waliona ni sawa tena baadhi wanatetea iongezwe zaidi ya hiyo. Hii imenijengea taswira kwamba upinzani upo kama danganya toto tu katika nchi hii wote ni wachumia tumbo; wananchi wasidanganyike kwamba kuna watu wanawatetea! Wajipange kisaikolojia kupambana na maadui wa tatu wa binadamu.
Ndugu Tambua kinachotesa hapa hi Mfumo uliopo kiuhalisia kutoa shutuma kwa Wapinzani si sahihi kwani wao kwanza kabisa wapo 10% ya wabunge wote waliobaki wote ni wa CCM ambao wanataka kuongezewa hizo posho, kwa swala hili ni vema tukaangalia katika hizi pande mbili.
1. Kama wabunge wanataka kuongezewa Posho je ni nani anaetaka kuwaongezea hizo posho? na fedha zinatoka wapi? na je Bunge hili halikuwa na bajeti mahususi ?

2. Sisi wanachi tunalichukuliaje suala hili je tuendelee kujadiliana katika mitandao na mwisho wa siku tunalala tu na tukiamka ni mwendelezo wa kulalamika kwenye mitandao?

Tambua hii kitu ilitokea Kenya pale Bunge lilipotaka kujiongezea Posho lakini wenzetu hatua zilichukuliwa ambazo ni
1. Rais Kenyata aligoma ongezeko hilo
2. Wananchi waliandamana hadi nje ya ukumbi wa Bunge kupinga Ongezeko hilo.
Sasa Tutafakari mimi na wewe Kama Kenyata kule Kenya alipinga ongezeko hilo hapa kwetu mbona Kikwete yupo Kimya? na pia sisi wananchi tunachukua hatua gani? kwani wenzetu Kenya waliandamana lakini huku kwetu kwa sasa tukiandamana itasemekana ni CHADEMA na mabomu yatapigwa kwa kwenda mbele
 
Kwahiyo tuseme wewe msimamo wa Chadema kuhusu posho hujausikia au ni kwa sababu kuzungumzia kuhusu posho ndo imekuwa habari ya mjini
 
Kuna wapinzani wachache wako kizalendo kuhusu hizo posho. wapo waliojitokeza kupinga kuongezwa kwake lakini wengi wao wamekaa kimya kutoonesha misimamo yao. binafsi natafsiri wote waliokaa kimya wanataka waongezewe.
Kwahyo unataka watu zaidi ya 90 kila mmoja aje hapa JF aseme mimi fulani napinga kuongezwa posho, Please hebu tuacheni kujadili kama vile tunalazimishwa
 
- Yaani Rais ashuke chini mpaka kwenye haya mambo na wakati Kamati ya Bunge ipo? Haiwezekani!!

Le Mutuz

Mi ningekuwa raisi matumizi yeyote yanayozidi bilioni moja kwa jambo moja lazima yangekuwa na "baraka" zangu... hususani tunapokuwa na viongozi walafi kama sasa...
Maana raisi ndiwe unazunguka nchi nzima wakati wa kampeni ukiahidi maji, barabara, zahanati, shule nk ambavyo utekelezaji wake ni function ya fedha za kodi na mapato mengine.
Lakini sasa unapokuta hela zinapatikana huko juu alafu zinaishia mifukoni mwa akina anonymous hapa kati kati... no way... ningekuwa raisi wacha tu nionekane mnoko but hela ikiidhinishwa kwenda kuchimba kisima, hakyanani nitaifuatilia hadi senti ya mwisho na ole wake atakayetafuna hata sh mia...
 
W. J. Malecela
Hoja yako ni ya msingi sana; hawa wajumbe kuwapa laki 3 kwa siku ni nyingi sana ukitilia maanani bajeti yetu 50% ni mikopo leo wameona haitoshi cha kuwashauri ni wajitoe naamini wapo watu wenye uchungu wataifanya hiyo kazi bure kwa maslahi ya taifa; ukweli uliopo katiba hiyo ya kuandaliwa na kundi ambalo limeweka maslahi yao mbele haitakidhi maslahi ya taifa ni kupoteza pesa za walipa kodi; wananchi ndio wenye sauti ya mwisho kwenye maamuzi ya katiba; wanasiasa wetu wanapaswa kuiga mifano inayotokea duniani mfano ni Ukraine katiba ya kupendelea chama kilichopo madarakani sio suluhisho la muda mrefu; wanaanchi wakidai haki yao hakuna risasi wala kifaru kitachowazuia; CCM ni chama kinachokubalika kinachotakiwa kufanywa na wanasiasa wetu ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo; hatukuhitaji kuunda tume wala bunge la katiba kwa mabilioni ya pesa ambayo yangetumika kuondoa kero za mwananchi wa kawaida
 
Back
Top Bottom