MlekwaKik
Member
- May 18, 2022
- 8
- 6
Kikwazo kikubwa cha uwajibikaji na utawala bora katika nchi yetu ni malezi anayopitia mtanzania wa kawaida, kuna namna ambavyo malezi yetu kuanzia shuleni hadi nyumbani yanatengeneza vijana waongo, wanafiki, wabinafsi na waoga. Maisha yetu kuanzia tukiwa watoto mpaka tunakuwa watu wazima ili uwe mtu wa kawaida uweze kuishi maisha ya kawaida ya kukubalika na wengi basi uwe na chembe za uongo, uoga na unafiki.
Mtoto wa kawaida wa kitanzania anatafsiri uoga kuwa ni heshima tangu akiwa nyumbani, na mtoto anaejiamini na kusema vitu kama vilivyo hata mbele ya wakubwa huwa jamii nzima inamuangalia kama mtoto mkorofi na asiekuwa na adabu. Hata kama anayoyasema hayajavunja maadili yoyote ila kitendo cha kujiamini kwa mtoto hutafsiriwa kuwa ni kukosa heshima. Mtoto anafundishwa kuwa muongo na muoga ili kuonekana ana heshima kwa wakubwa. Na anakuwa akitafsiri hivyo, kwamba kujiamini na kusema ukweli na kusimamia anachokiona kuwa ni sahihi, ni ukosefu wa adabu na heshima.
Analelewa hivi na wazazi wake na shuleni pia. Shule tulizopita ni mwiko kutoa mawazo yako tofauti na kile ambacho mwalimu anakijua au tofauti na mtaala wa elimu. Hata ukienda chuo kikuu kuna peer reviewed papers kwamba mawazo yako ni lazima yawe ndani ya mitazamo ya wasomi wengine. Tunafundishwa ubinafsi na kushindana tangu kwenye familia zetu na shuleni pia, anaefanya vizuri sana huwa anasifiwa na anaefanya vibaya huwa anasemwa kwa kuambiwa angalia wenzako.
Sasa matokeo ya haya yote yanakuja kuathiri mifumo yetu ya kiuongozi na taasisi zetu. Tunaandaa watu kuwa waongo, waoga, wanafiki na wabinafsi lakini tunadai utawala bora na uwajibikaji katika serikali na taasisi zetu. Mtu ambae amefundishwa kuwa uoga ni heshima akiwa Kiongozi usitegemee aweze kukubaliana na mazingira ya yeye kukosolewa au kuambiwa anakosea wapi, lazima atatafsiri hilo kuwa ni kudharauliwa.
Na matokeo yake ni kuweka mfumo ambao unaminya utawala bora. Mtu ambae alifundishwa kuwa mnafiki mbele ya wazazi na walimu na kufanya mambo mema pale tu ambapo wakubwa wanamuangalia usitegemee awe muwajibikaji akiwa kiongozi maana alifundishwa kuwa mnafiki na kufanya vitu vizuri mbele za watu. Malezi yetu yanatuandaa kuwa watu ambao sio wa kweli hata na sisi wenyewe na nafsi zetu. Ndo maana ni kawaida kwa mtanzania kufanya kazi kwa bidii boss akiwepo na kutofanya chochote akiwa mwenyewe. Tunashindwa hata kuwa waaminifu katika matumizi ya pesa zetu wenyewe, kwasababu hatujaandaliwa kuwa wawajibikaji kama tabia yetu.
Tunapoingia kwenye siasa zetu tunataka watu wawajibikaji na wanaoheshimu utawala bora, wanatoka wapi hao. Mtoto mdogo akiiba kitu alafu akaulizwa na watu wazima kwanini aliiba akisema ukweli atachapwa kwamba na anasema kwa kujiamini kabisa kwamba aliiba, bila kujua kuwa tunaua ile tabia ya kusema ukweli. Na ukiangalia unagundua kuwa siasa zetu pia zimejengwa katika misingi ya malezi tunayopitia tangu tukiwa watoto wadogo. Ni kawaida kuona mtu anasema uongo au anakuwa mnafiki mbele ya viongozi wa serikali au vyama vya siasa, ikitafsiriwa kwamba ni heshima na hao Viongozi. Ila akisema ukweli huwa inaonekana ni jeuri na dharau kwa viongozi.
Ubinafsi unaathiri utawala bora na uwajibikaji kwasababu hatufundishwi athari za matendo yetu mabaya kwa wengine, bali wazazi na walimu walikuwa wabinafsi kwa kuandaa watoto watiifu ili kurahisisha kazi yao ya malezi. Matokeo ya hii ni kuja kuwa na viongozi ambao nao pia wanataka kuongoza watu wenye utii watakaofanya yale wanayotaka, bila kujali athari za matendo yao kwa watu wengine.
Hii inaenda kuathiri hata pale tunapofanya maamuzi huwa hatujali yataathiri vipi watu wengine kwasababu hatujaandaliwa kuangalia athari na matendo na maamuzi yetu kwa wengine. Kwa mfano mtoto akiiba kalamu ya mwenzake atachapwa kwa kitendo cha kuiba na ataitwa mwizi, lakini hatafundishwa kuwa unapoiba kalama mwenzako hataweza kuandika.
Matokeo yake ni kwamba ataacha kuiba kwasababu anaogopa kuchapwa ila sio kwasababu akiiba wizi unaathiri wengine, huyu akipata tena fursa ya kuiba lazima ataiba tena. Na akiwa Kiongozi ataweka mazingira ya kuiba na hatakubali kusemwa ataweka mfumo wa kutosemwa na atatunga sheria za kuandaa watu wa kumtii na kumuogopa na hao watakuwa ndo wenye kufaa kwake kwasababu alifaa kwa wazazi na walimu kwa kuwa muongo, mnafiki na muoga, akasifiwa kuwa ni mtoto mzuri.
Hapa ndo tunapoona mtu anaweza kuiba dawa hospitali bila kuhofia labda hicho kidonge kimoja kinaweza kisikamilishe dozi ya mtu na kumletea umauti.
Utawala bora na uwajibikaji hauwezi kuangaliwa katika serikali au taasisi au vyama vya siasa, bali tuanze kuangalia katika ngazi ya malezi ya watoto katika familia zetu. Tuwafundishe watoto wetu kuwa wa kweli, wawe wanaojiamini na kusema yale wanayofikiri bila kumkosea mtu heshima, tuwafundishe watoto kuacha tabia zisizofaa sio kwa ubaya wa hizo tabia bali pia waambiwe namna matendo yao yanavyoweza kuleta madhara kwa wengine.
Na wafundishwe kwamba duniani patakuwa mahali salama kama tutawajibika katika kuwatumikia wengine na kuhakikisha tunajenga tabia ya kutatua changamoto na sio kuishi kwa kutafuta kumfurahisha Baba au Mama kwani hii wanaenda nayo mpaka ukubwani. Wanakuwa sio watoto wanaowajibika katika kuondoa changamoto za wengine bali watu wa kutafuta kumfurahisha Boss na yule mwenye mamlaka juu yao. Hii kitu inaua na kuondoka kabisa ile dhana ya uwajibikaji na utawala bora katika jamii yetu.

Upvote
1