mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Marekani ni mnunuaji mkubwa sana wa mafuta yasiyosafishwa toka Urusi!! Hilo ni eneo nyeti sana kwake kiuchuni. Jana katika hotuba yake muhimu kwa Taifa, mataifa ya ulaya yalitegemea Biden kutangaza kususia ununuaji wa mafuta toka Urusi, na kwa mshangao wao hakugusia kabisa jambo hilo. Hata baadhi ya wabunge wa Democratic wameshangaa na kuamua kuandika barua ya kumkosoa Biden na bado Biden kala jiwe!
Marekani haiko tayari kuweka vikwazo ambavyo itajikuta inaumia sana pia kiuchumi, lakini inazikomalia nchi za ulaya kuiwekea vikwazo Urusi bila kujali zitaumia namna gani!! Hilo ndilo beberu baba lao! Mataifa ya India, China, Pakistani, Brazil, Mexico yamegoma wazi wazi kuunga mkono vikwazo dhidi ya Urusi ili mradi tu kuifurahisha Marekani!! Yameamua kuzingatia maslahi yao!
Huko tunakokwenda, si ajabu Marekani ikaanza kuzilazimisha nchi zetu hizi kuunga tela dhidi ya Urusi!! Tukifikia huko, kuna mwenye ubavu kama wa Baba wa Taifa mwalimu Nyerere wa kusimama kidete na kusema SISI HATUFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE? Karibuni tudadavue!