Unafungua daftari la michango ya rambirambi unakuta mtu wa kwanza kaandika 1,200,000/=

Unafungua daftari la michango ya rambirambi unakuta mtu wa kwanza kaandika 1,200,000/=

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Good afternoon jamiiforums

Kumpa mfiwa pesa mkononi au kuandika kwenye daftari ni kipi bora zaidi emotionally? Jenga picha umeenda kwenye msiba wa baba yake rafiki yako sasa umefungua daftari la rambirambi unataka kuandika mchango wako wa 10,000/= mara ghafla unakutana na jina la mtu wa kwanza (sijui ni boss wa marehemu) amechangia 1,200,000/= unafanyaje? Yamenikuta sana haya miaka ya 2011 - 2017.

Unaweza ukajikuta unarudisha daftari la michango na kumuuliza mwenyeji wako "Frank, eti washroom ndio wapi?"

Mara nyingi nilipokuwa ninakutana na hali kama hii nilikuwa ninaamua kutokuandika kabisa katika daftari kisha ninaenda kwenye magenge ya hapo jirani na kununua nyanya, vitunguu na unga wa ugali kilo kadhaa au mikate ya waombolezaji kunywea chai asubuhi.

Nilikuwa ninaona aibu sana kuandika mchango mdogo wakati majina matatu ya juu wa kwanza ni 1,200,000, wa pili 900,000 na wa tatu 700,000/= alafu wa nne ndio niwe mimi na 15,000/= yangu? Hapana aisee bora nikampe mfiwa pesa mkononi.

Kuna mzee mmoja alikuwa ni dereva katika kampuni moja niliyokuwa ninafanyia kazi nilikuwa ninamuitaga mzee Juma.

Mzee nilimsimulia namna ambayo nimekuwa nikikutana na hali kama hii akacheka sana akniambia, babu hayo majina ya mwanzo ya waliochangia pesa kubwa huwa yanawekwa kwa makusudi ili kuhamasisha hawa wa chini wachangie nyingi pia kwa aibu.

Najua JF imejaa wamama na wababa wenye umri mkubwa (above 45) ambao wamepitia sana hali ya kubeba changamoto hizi za misiba majumbani mwao na wanaweza kutuambia kama ni kweli yale majina ya mwanzo yanatumiaka kama hamasa ama la. Ninaomba kuelimishwa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kaandika tu huyo kama mkwara. Je, una ushahidi kwamba alitoa kiasi hicho? Kuandika kiasi hicho na kutoa ni vitu viwili tofauti.
 
Hata ukitoa mchango wa 5000 itatumika tu kwenye shuguli
Mara nyingi nilipokuwa ninakutana na hali kama hii nilikuwa ninaamua kutokuandika kabisa katika daftari kisha ninaenda kwenye magenge ya hapo jirani na kununua nyanya, vitunguu na unga wa ugali kilo kadhaa au mikate ya waombolezaji kunywea chai asubuhi.
 
Mkuu, 5000 ni ya kumpa mfiwa mkononi au ya kuandika kwenye daftari
Hata kwenye daftari unaandika tu mzee
Toa ulichonacho

Waswahili husema ya kwamba, "uso umeumbwa na haya"
Hutakiwi kuwa na haya mzee mimi nishawahi kudai changu kwa marehemu,walipouliza tu kuna anayemdai marehemu nkatokeaa
Hutakiwi kuwa na haya mzee kwenye maisha

Ova
 
Lile taftari siyo la kulikimbilia linahitaji timing, mara nyingi jina la kwanza huwa wanaandika namba kubwa(hewa) ili wanaofuata waone aibu angalau wapandepande,mbona kitaa wadau tunalijua hilo kitambo.
 
Back
Top Bottom