Niliwahi kupata rafiki mmoja miaka ya 2007 mbezi beach, jamaa kwa jina alikua anaitwa F yeye ni mkristo, jamaa alikuwa mshikaji wangu kwa saana na sababu kubwa mshikaji alikuwa na akilinya kutafta pesa yaan hawezi kaa bila pesa, jamaa kuna siku alinipa mchongo wa kupiga pesa ( ki tapeli tapeli hivi ) dah mimi mwanzo sikuafikiana nao kabisa, lakini jamaa akasisitiza pale kuna pesa, dah nikaona sio kesi ngoja nimdikilize ili nione hiyo pesa itakujaje, basi akaniuliza kama nna elfu 40 nikamwambia nnayo akasema twende stationary, tukaenda, akadraft kitu kimoja sitokuja kusahau, yaani yule mpuuzi alitengeneza likitu flani la kuomba michango kumhusu padri mmoja ambaye alikuwa akisali kwenye kanisa hilo la huyo padri ( simjui huyo Padri anamjua yeye mwenyewe maana hata mambo ya kanisa siyajui, basi kwenye zile karatasi kulikuwa na kitu kama upadrisho, sikujua alidhamiria nini ila mimi nilitaka kuona hiyo pesa tu inapatikanaje na zaidi pesa yangu elfu 40 niliyotoa kama mtaji wa utapeli wake.
Baada ya kumaliza zile karatasi ambazo zilikuwa na jina la hiyo padri sahihi na mhuri jamaa akaniambia sasa mzee twende tukappige hela, pembeni huku kulikuwa na sehemu kama ya kujaza hivi yaan anauetoa ule mchango anajaza ile forum na sahihi yake na namba zake za simu, tukaanza kupita sasa kwenye magate ya watu wanene ambao yeye anawajua wanasali katika lile kanisa, akitoka beki 3 anaulizwa boss wako yupo? Kama yupo tunakaribishwa ndani, kama hayupo tunaacha ile bahasha ya mchango, zile karatasi zilikuwa na majina ambayo zilikuwa zimeshajazwa wa kwanza mpaka wa tano ingine wa tatu, basi pale juu unaandika flan bin flan yeye katoa laki, sasa ma buda wa kule wanapenda ushindani, akiona jirani yake katoa laki yeye anatoa laki na nusu ama laki pia,
Siku ya kwanza tulipata laaki saba, hapo kwenye karatasi kumi na moja za mwanzo, na jamaa alitoa copy karatasi 190..basi jioni kwenye mgao mimi akanipa laki mbili yeye akabaki na laki nne, ukitoa na ile 40 yangu ya mtaji na chakula na kidang'a
Nilifikiria hii mbinu nikaona hapana, huu ni utapeli, ippo siku nitaingia kwenye 18 za watu, nikamwambia ndugu mimi naona tuishie hapa sababu huu ni utapeli, akasema fresh mm nimekupa mchongo sababu wewe ni mchizi wangu, sema wewe ni mpumbavu tena mpumbavu k*****ko! Doh, jamaa alikuwa kanizodi umri, nikaona sio kesi mm nikakausha,
Kesho yake asubuhi kanitimbia home, we fala twende zetu, dah mimi nikajikusanya nikabeba leseni yangu, kipindi hicho class D ya kitabu, hao tukkaingia mzigoni kupitia mtonyo, kama sijakosea ilikiwa jumamosi, tukapita mageti tunagonga kuulizia kama wale tuliowaachia zile fomu wamezifikisha kwa wahusika, tukapata kama laki tatu hivi, sasa kuna nyumba moja kuubwa hivi ima ukuta mrefu mno, ipo jirani na mzee flani maarufu sana, tumefika pale kugonga fasta mlango ukafunguliwa, ndani naona ile mijibwa kama ya polidi ipo minne alafu kuna mzee mmoja kajaza kinyama anamwagia bustani na watoto wake wakike pini kinyama wanapata kifungua kinywa bustanini, fasta akili ikaniambia usiingie humo ndani, nikamstua jamaa, oya mi machale yananicheza tusiingine jamaa alinijibu jibu moja tu, we "a nini, tumalizie hapa alafu kuanzia leo tusijuane, nikamwambia k mwenyewe we huoni hatari hii wakati tunajibizana buda akaja mwenyewe getiti karibuni vijana, piteni ndani wanangu ujumbe wenu nimeupata, dah, tukaingia, lango likafungwa, tukakaribishwa pale bustanini,
Mmekunywa chai? Jamaa yangu akajibu bado, mzee akasema wakaangieni mayai kumi hawa vijana mimi hapo akili yangu inatafta penye ukuta mfupi ikiwezekana kama kuna lolote litokea nifanye kama maninja maana moyo unadunda kinyama, yaani naisikia kabisa harufu ya hatari hatari mule ndani..
Kijana unaitwa nani? Nikajibu jina langu halisi, jamaa yangu akashangaa, akanikanyaga kwa chini ya meza, mi nikajibu jina langu tena lote, mzee akasema wewe ni Muislam eeh nikajibu ndio, do nikazidi mchanganya F, Mzee alipomaliza na mimi aliniambia kijana wewe ninmwerevu sana, una akili, akamgeukia F, enhe, F mtoto wa mzee flani, baba yako ni rafiki yangu sana, nimesoma nae Prof ........, Ni mtu wangu wa karibu sana.. akatumiminia juice na yeye akajimiminia.
Akarudi kwangu, kijana wewe elimu yako ipo vipi? Tufahamiane zaidi, niliposikia tufahamiane zaidi moja kwa moja nikajua leo nimeingia kwenye choo cha vilema, mkono ndala miguu ndala, harufu ya hatari ikajaa, nikajihisi kujutia uupuzi wangu wa kupuuza mambo hasa yanayohudisha maisha.
Nikasema elimu yangu na ujuxi wangu wa kuunga unga mwingine mwingine, mayai yakawa yameshaletwa, soseji na juice nyingine, nikaviangalia vile vitu, nikajikuta tu nasema dah! Hapo sasa tayari niko tayari kwa hatari ki akili na kimwili niko tayari kwa lolote na kufanya chochote kiwe kizuri ama vibaya nitoke mle ndani maana ile kengele ya hatari ikazidi kuhonga kichwani, mzee akamuagiza mtoto wake wa kike, naomba niletee laki moja na ile karatasi waliyoileta hawa vijana..
Nikamuona F yeye anakula huku anatabasamu ilhal mm tayar nainusa hatari, karatasi ikaja, na laki vikawekwa mezani alafu mzee juu ya ile karatasi akaweka bastola!
Akamwita F ,unanijua mimi ni nani? Shwali hili lilifanya F acheue ule mchanganiko wa Juice na mayai mdomoni, mzee kwa sauti ya utulivu akauliza mara ya pili, unanijua vizuri? Ama nijitambulisha? Nikaona F sasa anapiga magoti anaanza kuomba msamaha, nikaona hili ndo tulikuwa tunalitafuta, mzee akauliza huyu ambao mnatumia jina lake kujipatia pesa mnamfahamu vizuri,? Je mmeshawatapeli watu wote hawa? ( Kwenye list )
Kisha akasema hii haivumiki leo mtajifunza kitu.
Kwanza akabonyeza namba akampigia baba yake F, baba mzazi wa F Alipopokea niliskia tu anasema mkuu, wakasalimiana alafu yule mzee anavyojua kuwaua watu ma kihoro akamuuliza mzee wa F hivi yule kijana wako yupo wapi sasa hivi? Akamjibu yupo mbezi, akauliza alishaajiriwa? Foh baba mtu akatoa maelezo meengi kumbe yule msen*e watu wanampambania sema yeye tu ndio ngedere wa mtaa hajielewi, basi mzee wakaongea mambo yao akakata simu, akamtazama F
Haya leo mmefikia kwangu nafahamiana na baba yako je ukiingia kwa mwingine itakuwaje? Kwanini umeamua uwe tapeli? Wewe si una Elimu ya chuo kwanini hivi? Wewe kijana umeshindwa mshauri mwenzako? Kwanza mmekutana wapi? We Fred ndio mwenye shida unaonekana kabisa machoni, haya naombeni hizo pesa mlizotapeli tangu siku ya jana mpaka leo, kisha karatasi zote mziache hapa, we kijana ( lete leseni yako ntakusaifia kukutaftia kazi mahali, lakini wewe F nitabaki na wewe hapa, sababu huyu mlitumia jina lake kutapeli kwanza hayuko nchini, lakini uxuti anakuja leo, hivyo nataka nikukutanishe nae umalizane nae mwenyewe unaonaje? F akaanza kulia, nilippomuona analia kifogo nicheke....aaagh sitokuja kurudia ule ujinga! Wala sihitaji marafiki janja janja..
Tangu ile siku sikumuona F na nilihama mbezi.