Unafungua daftari la michango ya rambirambi unakuta mtu wa kwanza kaandika 1,200,000/=

Hyo huwa jambisha jambisha ili watu watoe kiasi kikubwa,back to me nilikuta jina la mwanangu ninayemfahamu kabsa eti katoa 100k nikasema aaaah wap...wakati huyo mwanangu mbahili wa kutupwa mpaka akitoa sadaka kanisani anachukua chenchi kwenye kikapu[emoji23][emoji23]
 
Mi nilikuwa na buku nikaandika 900.0 na chenji nikadai
 
Hiyo ni bosheni tu kuwafanya wasijielewa kuingia mkenge kufuata mkumbo [emoji108][emoji108][emoji108]
 
Kama uliwai kuhudhuria vikao vya harusi utakua unaelewa maana yake, Kwenye hivi vikao vya michango wanakuwepo waropokaji walioandaliwa wawe wa kwanza kutoa ahadi. Unashangaa anasimama mtu huko nyuma anachangia milion kadhaa, hawa wengine ni lazima wajiongeze, Lakini hawa waliondaliwa kuropoka si kweli kwamba wanatoa hizo ela walizoahidi hio inakua siri ya Kamati.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kwani Magige daftari lake mtu wa kwanza hadi tatu waliandika sh ngapi...

Misiba kwa mijini nayo imekuwa upigaji, ila kijijini mambo ya rambirambi ni mara chache sana
 
Rambi rambi haimpozi machungu mfiwa msibani
 
Hata kwenye kutoa zawadi utasikia mtu anasimama mbele anasema,nimejitolea kuwapa maharusi gari,kiwanja,nyumba kumbe ile ni uzushi tu😂😂

Ova
 
Unatoa hiyo 15,000 yako then unaongeza zero mbili mbele...
 
Kwanza jua Mazishi na Misiba ni ghali. Tofauti na wale wanaofukia lakini kwa tunaozika Mazishi ya kawaida sana na mwili haujasafirishwa ni milioni 5

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
..."Toa ndugu, toa ndugu,
Ulicho nacho Wewe,
Mungu atakuona, Mpaka rohoni mwako"...
 
Changia kwa uwezo wako, isikutishe kiasi alichochangia aliekutangulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…