Unafungua daftari la michango ya rambirambi unakuta mtu wa kwanza kaandika 1,200,000/=

Sasa na wewe unakuwaje wa kwanza kwanza hivyo kwenye kuchanga???
 
Sasa yanarudi mkuu, enzi za fanya kazi ndio upate pesa zimeenda na mwenye hiyo falsafa, sasa ni ongea maneno matamu ingiza mamilioni kilaini
 
Sasa yanarudi mkuu, enzi za fanya kazi ndio upate pesa zimeenda na mwenye hiyo falsafa, sasa ni ongea maneno matamu ingiza mamilioni kilaini
Wakati wa baba yetu JPM pesa ilikuwa ngumu sana kuipata.
 
Hata kwenye daftari unaandika tu mzee
Toa ulichonacho


Hutakiwi kuwa na haya mzee mimi nishawahi kudai changu kwa marehemu,walipouliza tu kuna anayemdai marehemu nkatokeaa
Hutakiwi kuwa na haya mzee kwenye maisha

Ova
Marehemu alikuwa ni mmasai nini?Sio bure.
 
Waswahili husema ya kwamba, "uso umeumbwa na haya"
Basi wewe kwenye maisha huenda unapata tabu sana. Siku zote mchango siyo mashindano. Unaweza kutoa sh. elfu kumi ikawa umejitoa zaidi ya mtu aliyetoa sh. milioni mbili. Kwenye maisha ukishanza kuishi maisha ya ku-fake uko juu kuliko kipato chako utaumia. Kwa wale wakristo wanajua maandiko haya kutoka kwenye biblia: Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.
 
Siku zote mchango siyo mashindano. Unaweza kutoa sh. elfu kumi ikawa umejitoa zaidi ya mtu aliyetoa sh. milioni mbili. Kwenye maisha ukishanza kuishi maisha ya ku-fake uko juu kuliko kipato chako utaumia.
Ni bora kumpa mkononi mfiwa pesa ndogo kuliko kuandika kwenye daftari
 
Niliona aibu nikaamua kumpa jamaa pesa mkononi
Kukubali maisha yako ni kitu muhimu sana, unayakubali halafu unakata mshipa wa noma.

Hususan kama umeshajaribu kuyabadili ukashindwa

Na wewe una utu ambao haupimwi kwa hela, mtu anaweza kutoa hela nyingi lakini akawa hana mawazo mazuri, hela ikawa haijasaidia.

Au huyo mwenye hela akawa yuko busy sana hawezi kusaidia kazi fulani, sisi wengine ambao hatuna hela sana ndio tukapiga kazi.

Yote maisha tu, unyonge mwingine utajipa mwenyewe bila sababu.

Mwaka 1998 nishawahi kutoa Sh 10,000 kwenye msiba nikajiona mnyonge sana kwamba natoa kidogo.

Baadaye ikaonekana hiyo 10,000 ndiyo ilikuwa kati ya watemi, kuna watu walitoa mpaka 500.

Lakini unaweza kuambiwa kuna mama katoa 500 halafu kafanya kazi kubwa sana ya kupika msibani.

Nyerere alitufundisha, "Utu wa mtu ni kazi, pesa ni matokeo".

Mzalendo nafikiri unayajua haya mambo, basi tu.
 
Asante mkuu, umefafanua vema sana. Thanks.
 
Asante mtumishi wa Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…