Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Nawe ni mtazamo wako sikushangaiNi mtazamo na fikra zako tu, nadhani wewe ndie unatakiwa kubadilika na kupewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya neno kambo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nawe ni mtazamo wako sikushangaiNi mtazamo na fikra zako tu, nadhani wewe ndie unatakiwa kubadilika na kupewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya neno kambo.
Ndiyo Sasa nimepata fursa ngoja niyakusanye sasa hivi nimpe kamishna wa ustawi anipe majibu nirudi hapa sasa nikupe. Mambo mengi ndugu zangu, kuna wakati napotea kuendelea na mengine narejea tena. Subiri tafadhali, shukraniVyema.
Ila bado kuna vijiswali pale juu.
Nasubiri Dkt aje kunifafanulia.
Utaratibu wa kuasili watoto mapacha unafana na watoto wengine. Kanuni ya kuasili 3(e) hairuhusiwi kuwatenganisha watoto ndugu.Dkt. Gwajima D
Ni wazo zuri sana na nimelipenda bila pasi na shaka.
Naomba kuuliza, je, utaratibu huo pia unahusisha katika uasili kwa watoto pacha?
Pia, katika vigezo vikuu vya kuasili, ni lazima kutakuwa na kimoja au viwili ambavyo viko strong na ndio mara nyingi ninyi kama wizara huwa mnaangalia kwa umakini sana.
Unaweza kubainisha vigezo vikuu?
Yamkini, ninajua hayo yaliyoorodheswa, ila hujasemea suala la umri, mazingira yapi ni rafiki sana kwa uasili wa mtoto/watoto.
Na je, naruhusiwa kuasili kuanzia watoto wangapi?
Na pia, hata wa kariba lingine mf. wa kikorea, wa kizungu etc, almradi tu nimemkuta kituoni?
Asante.
Hii ni habari njema sana, watu wengi walikuwa wanaisubiri kwa shauku kubwa sana ujio wa jambo hili.Wasaalam Wana Jukwaa wote.
Kwa aliyebarikiwa neema ya Kulea watoto kwa malezi ya kambo au kumuasili kisheria awe wake;
UTARATIBU;
Baada ya kuwasilisha maombi Halmashauri;
1. Afisa Ustawi wa Jamii atakutembelea na kufanya tathmini.
2. Taarifa itawasilishwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizarani.
3. Iwapo hakuna hoja pingamizi, Kamishna atatoa kibali kwa mwombaji kumtambua mtoto.
4. Afisa Ustawi wa Jamii ataendelea kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya familia iliyomtambua mtoto na kuanza kumlea malezi ya kambo.
5. Taarifa ya maendeleo ya malezi ya kambo baada ya mathalani miezi sita hivi itawasilishwa tena kwa Kamishna, kwa ajili ya kuthibitisha kuwa maendeleo ya malezi ya kambo ni mazuri, hakuna changamoto hivyo, kibali cha kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya Kuasili mtoto huyo kitatolewa.
Hakuna malipo yoyote epuka ulaghai wa wasio waadilifu.
I'll ukawafundishe ushoga ? Nitapambna kwa namna yoyote usipeww mtotoAhsantee sana Dkt, naamini ndoto ya kuja kuwa na watoto wa kuasili itatimia, ubarikiwe sana.
[emoji120][emoji120]
Haya mkuu.Ndiyo Sasa nimepata fursa ngoja niyakusanye sasa hivi nimpe kamishna wa ustawi anipe majibu nirudi hapa sasa nikupe. Mambo mengi ndugu zangu, kuna wakati napotea kuendelea na mengine narejea tena. Subiri tafadhali, shukrani
Asante sana mkuu,umenifumbua macho kwa yale ambayo nilikuwa sina uelewa nayo, hasa hili la mapacha, kumzidi miaka 21 pamoja na uraia mwingine kwa mtoto unayetaka kumuasili.Utaratibu wa kuasili watoto mapacha unafana na watoto wengine. Kanuni ya kuasili 3(e) hairuhusiwi kuwatenganisha watoto ndugu.
Kuhusu vigezo vikuu; vigezo vyote kuasili ni vikuu kwa ulinzi na usalama wa mtoto na ni njia mojawapo ya kujiridhisha kwamba mtu ametimiza vigezo
Umri wa kuasili mtoto ni umri wowote chini ya miaka 18. Kigezo cha umri pia kimewekwa kwa mwombaji wa kuasili. Sheria ya Mtoto kifungu cha 56(a) kinasema, mwombaji awe na umri wa miaka 25 kupanda na amzidi mtoto miaka 21. Mwombaji mwenye miaka 50 atapewa mtoto mwenye umri wa kuanzia miaka 10
Unaweza kuasili watoto wawili kwa wakati mmoja (kanuni iliyopo kwenye mapitio imepunguza idadi ya watoto kutoka 3 mpaka 2)
Tanzania haijaridhia uasili baina ya mataifa hivyo, watoto wanaoasiliwa ni Watanzania tu. Kama ni mtoto raia wa nchi nyingine sheria haijamtambua kwenye suala la kuasili (ipo kimya). Kwa watoto wa makabila ya Tanzania unaweza kuasili mtoto wa kabila lolote.
Shukrani sana kwa mchango wako kwenye mjadala huu. Iko siku tutawaleta wataalamu kwenye mkutano online Ili mpate elimu na ufafanuzi mpana zaidi.
Yaan ushinde na kitaulo cheupe tu siku nzima au SIO?Mimi ni baba mtu mzima, nahutaji jimama wa Kuni adopt
Naona Dkt. Gwajima D ameamua kushusha nondo za ustawi wa jamii. #2025 imekaribia, yaani ni balaa tupu 😂Noma sana!