Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Sitaki kuamini kuwa ndiye alisema wametest mitambo
Nahisi waliamua kumharibia tu
Muda ni Mwalimu mwema kwa Kila swali. Tuzidi kupambanua kile Mungu ameweka ndani yetu, muda wetu ni mfupi na unapita kasi, saa inakuja ya kuuona uso wake na kupimwa kwa mizani yake. Nakutakia Heri na Baraka za Mungu. 🤝
 
Wasaalam Wana Jukwaa wote.

Kwa aliyebarikiwa neema ya Kulea watoto kwa malezi ya kambo au kumuasili kisheria awe wake;

UTARATIBU;

Baada ya kuwasilisha maombi Halmashauri;

1. Afisa Ustawi wa Jamii atakutembelea na kufanya tathmini.

2. Taarifa itawasilishwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizarani.

3. Iwapo hakuna hoja pingamizi, Kamishna atatoa kibali kwa mwombaji kumtambua mtoto.

4. Afisa Ustawi wa Jamii ataendelea kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya familia iliyomtambua mtoto na kuanza kumlea malezi ya kambo.

5. Taarifa ya maendeleo ya malezi ya kambo baada ya mathalani miezi sita hivi itawasilishwa tena kwa Kamishna, kwa ajili ya kuthibitisha kuwa maendeleo ya malezi ya kambo ni mazuri, hakuna changamoto hivyo, kibali cha kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya Kuasili mtoto huyo kitatolewa.

Hakuna malipo yoyote epuka ulaghai wa wasio waadilifu.
Dr shikamoo! Samahani niulize kabla sijapatiwa mtoto je nitaruhusiwa kujichagulia aina ya mtoto kwa maana ya jinsia? Umri? Mwonekano? Na nikiomba historia ya mtoto nitapatiwa? Au mimi nitapatiwa mtoto tu kwa matakwa ya afsa ustawi wa jamii? Asante.
 
Ahsante kwa swali zuri. Ukishapewa kibali, unaenda mwenyewe kuchagua ukiongozwa na Afisa Ustawi wa Jamii. Taarifa stahiki muhimu utapewa huko huko.
 
Ahsante Sana kufuatilia mjadala huu na kuchangia. Tumetoa namba hizo za call center za wizara Ili kama ikitokea tumechelewa kuona hapa basi fuatilieni kwenye namba hizo.

Ufafanuzi kwa ufupi;

1. Sheria imeruhusu kuasili mtoto wa umri wowote ila limitation ya umri imewekwa kwa waombaji/adoptive parents (mwombaji mwenye umri wa kuanzia miaka 50 ataruhusiwa kuasili mtoto wa kuanzia miaka 10 na mwisho wa kufanya applications ni miaka 65).

2. Ikitokea mzazi amejitokeza kwa ajili ya kuasili, Mahakama ndiyo imepewa mamlaka hivyo, atawasilisha kesi yake Mahakamani ambapo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii atashirikishwa kwenye kufanya tathmini kwa sababu ndiye aliyetoa kibali cha kuwasilisha shauri Mahakamani baada ya kipindi cha malezi ya Kambo kwisha.

3. Ikumbukwe, kabla ya kuruhusu mtoto kuwekwa kwenye malezi ya Kambo Afisa Ustawi wa Halmashauri amepewa jukumu la kufanya uchunguzi wa kina kwa ushirikiano na Polisi ili kujidhirisha kwamba hakuna mzazi na kama Kuna mzazi ridhaa ya kisheria inatakiwa ya mzazi ila wakati mwingine kutegemeana na mazingira ya mzazi au mlezi Kamishna au Mahakama inaweza isihitaji ridhaa mfano, kama mzazi ana changamoto ya afya ya akili au amemtelekeza mtoto.

Kuhusu IVF; mpaka Sasa suala la IVF au surrogacy haijaingizwa kwenye Sheria ya Mtoto. Tutawasiliana na wizara husika.

Shukrani, [emoji1431]
Nina swali
Sijaoa bado ila tu assume sioi kabisa. Je sheria inaruhusu ku adopt mtoto/watoto kama sijawai oa/sina mke?
 
Coca wangu usiondolewe kwenye reli na huyo nyamkomwe mwenye wivu.

Ongea na Dokta Gwajima ukajichukulie katoto kako ukalee. Ni heshima mno.

Utaratibu umeshawekwa. Ni wewe tu.

Akiiii tumbo langu la uzazi limecheza, isingekuwa nazaa basi ningeenda na mie kujinyakulia katoto kangu ka kambo.
Mnachafua uzi 🤣 🤣
 
Ahsante Sana kwa swali zuri. Kwa sasa sheria iliyopo hairuhusu mwanaume.

Toa maoni yako tafadhali
Anae ruhusiwa ku asili mtoto ni mwanamke pekee? (Au sijaelewa)

Kama ni hivyo inahitaji mabadiliko na maboresho, kuna wengine swala la ndoa limetupita kushoto mno ,mnapaswa kujua na sie tupo kuliko kuongeza idadi ya single mothers mtaani ni bora huu mlango ufunguliwe
 
Wakati ule ikitungwa sheria iliyopo ilikuwa hivyo, ila sheria zote hubadilika kwa nyakati kulingana na maoni ya watumiaji wa sheria na taarifa za kitafiti na uzoefu mbalimbali. Hivyo, tunapokea maoni. Shukrani
 
Asante Dr. Kwa mada nzuri...

Naamini utasaidia wengi kwa utaratibu huu...

Naomba urahisishe utaratibu wa kupima DNA pia...

Maana kesi ni nyingi halafu utaratibu wa kupima ni mgumu...

Ni jambo jema kulea mtoto asiye wako kwa kupenda si kwa kudanganywa.
Ahsante Sana kwa maoni. Kwa kuwa huduma hiyo Iko wizara ya afya, tutaratibu kikao cha mashirikiano kuwasilisha maoni haya. Naomba tu muwe critical, Changomoto Iko eneo gani la huduma hiyo tafadhali
 
Wakati ule ikitungwa sheria iliyopo ilikuwa hivyo, ila sheria zote hubadilika kwa nyakati kulingana na maoni ya watumiaji wa sheria na taarifa za kitafiti na uzoefu mbalimbali. Hivyo, tunapokea maoni. Shukrani
Nimeona inasema kwa mwanaume lazima iwepo sababu maalumi

Kama sheria ililenga kumlinda mtoto na domestic violence, sidhan kama jinsia Me ni hatari kuliko jinsia Ke kwenye hili eneo , ni rare cases utakuta mtoto/mtoto wa kambo au hata dada wa kazi anateswa na baba, most of the time ni jinsia Ke , hili waziri liangalie vizuri , sisi wanaume tunajulikana kwa kusumbua wake zetu sio hivyo vi malaika, mliempa dhamana kwasasa ndie hatari zaid
 
Ahsante Sana kufuatilia mjadala huu na kuchangia. Tumetoa namba hizo za call center za wizara Ili kama ikitokea tumechelewa kuona hapa basi fuatilieni kwenye namba hizo.

Ufafanuzi kwa ufupi;

1. Sheria imeruhusu kuasili mtoto wa umri wowote ila limitation ya umri imewekwa kwa waombaji/adoptive parents (mwombaji mwenye umri wa kuanzia miaka 50 ataruhusiwa kuasili mtoto wa kuanzia miaka 10 na mwisho wa kufanya applications ni miaka 65).

2. Ikitokea mzazi amejitokeza kwa ajili ya kuasili, Mahakama ndiyo imepewa mamlaka hivyo, atawasilisha kesi yake Mahakamani ambapo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii atashirikishwa kwenye kufanya tathmini kwa sababu ndiye aliyetoa kibali cha kuwasilisha shauri Mahakamani baada ya kipindi cha malezi ya Kambo kwisha.

3. Ikumbukwe, kabla ya kuruhusu mtoto kuwekwa kwenye malezi ya Kambo Afisa Ustawi wa Halmashauri amepewa jukumu la kufanya uchunguzi wa kina kwa ushirikiano na Polisi ili kujidhirisha kwamba hakuna mzazi na kama Kuna mzazi ridhaa ya kisheria inatakiwa ya mzazi ila wakati mwingine kutegemeana na mazingira ya mzazi au mlezi Kamishna au Mahakama inaweza isihitaji ridhaa mfano, kama mzazi ana changamoto ya afya ya akili au amemtelekeza mtoto.

Kuhusu IVF; mpaka Sasa suala la IVF au surrogacy haijaingizwa kwenye Sheria ya Mtoto. Tutawasiliana na wizara husika.

Shukrani, 🙏🏽
Asante kwa majibu mazuri.
Tunaomba mrejesho kuhusu IVF baada ya kufanya mawasiliano na Wizara husika sababu jambo la IVF linafanyika ndani ya nchi kwa zaidi ya miaka kadhaa sasa bila muongozo wowote wa kisera na kisheria toka Serikalini na Wizara husika ikizingatiwa kwamba hiyo ni Technologia mpya ya kimatibabu ya uzazi kwa Tanzania.
 
Anae ruhusiwa ku asili mtoto ni mwanamke pekee? (Au sijaelewa)

Kama ni hivyo inahitaji mabadiliko na maboresho, kuna wengine swala la ndoa limetupita kushoto mno ,mnapaswa kujua na sie tupo kuliko kuongeza idadi ya single mothers mtaani ni bora huu mlango ufunguliwe
Njoo uchukue mtoto mkuu wapo.
 
Ahsante Sana kwa maoni. Kwa kuwa huduma hiyo Iko wizara ya afya, tutaratibu kikao cha mashirikiano kuwasilisha maoni haya. Naomba tu muwe critical, Changomoto Iko eneo gani la huduma hiyo tafadhali
Kama nimemuelewa alichotaka kumaaanisha, huduma ya DNA iwe mandatory on delivery, mtoto akizaliwa tu hapo hapo mzigo apewe baba husika kwa majibu ya DNA , au mtu akiamua kumlelea alelee kwa hiyari yake mwenyewe na sio kubambikiziwa
 
Njoo uchukue mtoto mkuu wapo.
Sheria mzee, ndio nauliza, nimeisoma naona inatoa room kwa special case. Sasa special case sijui n nn, ningetaman kuchukua hata wawili , mmoja Me mwingine Ke
 
Dkt. Gwajima D
Ni wazo zuri sana na nimelipenda bila pasi na shaka.
Naomba kuuliza, je, utaratibu huo pia unahusisha katika uasili kwa watoto pacha?

Pia, katika vigezo vikuu vya kuasili, ni lazima kutakuwa na kimoja au viwili ambavyo viko strong na ndio mara nyingi ninyi kama wizara huwa mnaangalia kwa umakini sana.
Unaweza kubainisha vigezo vikuu?
Yamkini, ninajua hayo yaliyoorodheswa, ila hujasemea suala la umri, mazingira yapi ni rafiki sana kwa uasili wa mtoto/watoto.
Na je, naruhusiwa kuasili kuanzia watoto wangapi?
Na pia, hata wa kariba lingine mf. wa kikorea, wa kizungu etc, almradi tu nimemkuta kituoni?

Asante.
 
Dkt. Gwajima D
Ni wazo zuri sana na nimelipenda bila pasi na shaka.
Naomba kuuliza, je, utaratibu huo pia unahusisha katika uasili kwa watoto pacha?

Pia, katika vigezo vikuu vya kuasili, ni lazima kutakuwa na kimoja au viwili ambavyo viko strong na ndio mara nyingi ninyi kama wizara huwa mnaangalia kwa umakini sana.
Unaweza kubainisha vigezo vikuu?
Yamkini, ninajua hayo yaliyoorodheswa, ila hujasemea suala la umri, mazingira yapi ni rafiki sana kwa uasili wa mtoto/watoto.
Na je, naruhusiwa kuasili kuanzia watoto wangapi?

Asante.
Kuhusu umri wewe muombaji unapaswa kua na miaka 25 na kuendelea na age difference ya miaka 21 walau
 
Ahsante Sana kwa maoni. Kwa kuwa huduma hiyo Iko wizara ya afya, tutaratibu kikao cha mashirikiano kuwasilisha maoni haya. Naomba tu muwe critical, Changomoto Iko eneo gani la huduma hiyo tafadhali
Asante kwa kunipa mda japo mada yangu haiko kwenye wizara yako...

Changamoto iko kwenye utaratibu wa kupita hadi kufika kwenye vipimo...

Kwanini utaratibu usiwe rahisi, kwamba mtu akitaka kupima aende hospitali moja kwa moja kuliko ilivyo sasa hadi mtu apitie polisi au kwenye dawati la jinsia? (niko tayari kusahihishwa)
 
Back
Top Bottom