Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Ni ndoto yangu kuwa sehemu ya jamii kuwainua watoto walio kwenye mahitaji na changamoto za kimaisha.
Hilo la kuasili nimewahi kulifikiria lakini nikifikiria umuhimu wa nasaba kwakeli naona sio bora sana kumchukua mtoto wa mtu damu ya mtu kuifanya iwe damu yako, labda sipo sahihi.
 
Asante sana Mheshimiwa. Nilishaanza malezi ya kambo bila kufuata huu utaratibu. Nitaenda ofisi za ustawi wa jamii kufuata utaratibu.
 
Wasaalam Wana Jukwaa wote.

Kwa aliyebarikiwa neema ya Kulea watoto kwa malezi ya kambo au kumuasili kisheria awe wake;

UTARATIBU;

Baada ya kuwasilisha maombi Halmashauri;

1. Afisa Ustawi wa Jamii atakutembelea na kufanya tathmini.

2. Taarifa itawasilishwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizarani.

3. Iwapo hakuna hoja pingamizi, Kamishna atatoa kibali kwa mwombaji kumtambua mtoto.

4. Afisa Ustawi wa Jamii ataendelea kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya familia iliyomtambua mtoto na kuanza kumlea malezi ya kambo.

5. Taarifa ya maendeleo ya malezi ya kambo baada ya mathalani miezi sita hivi itawasilishwa tena kwa Kamishna, kwa ajili ya kuthibitisha kuwa maendeleo ya malezi ya kambo ni mazuri, hakuna changamoto hivyo, kibali cha kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya Kuasili mtoto huyo kitatolewa.

Hakuna malipo yoyote epuka ulaghai wa wasio waadilifu.
Asante sana Dkt. Keep it up!
 
Sasa mashoga wamefanyajee? Wao hawaruhusiwi kuasili mtoto? Khaaah
Coca wangu usiondolewe kwenye reli na huyo nyamkomwe mwenye wivu.

Ongea na Dokta Gwajima ukajichukulie katoto kako ukalee. Ni heshima mno.

Utaratibu umeshawekwa. Ni wewe tu.

Akiiii tumbo langu la uzazi limecheza, isingekuwa nazaa basi ningeenda na mie kujinyakulia katoto kangu ka kambo.
 
Wasaalam Wana Jukwaa wote.

Kwa aliyebarikiwa neema ya Kulea watoto kwa malezi ya kambo au kumuasili kisheria awe wake;

UTARATIBU;

Baada ya kuwasilisha maombi Halmashauri;

1. Afisa Ustawi wa Jamii atakutembelea na kufanya tathmini.

2. Taarifa itawasilishwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizarani.

3. Iwapo hakuna hoja pingamizi, Kamishna atatoa kibali kwa mwombaji kumtambua mtoto.

4. Afisa Ustawi wa Jamii ataendelea kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya familia iliyomtambua mtoto na kuanza kumlea malezi ya kambo.

5. Taarifa ya maendeleo ya malezi ya kambo baada ya mathalani miezi sita hivi itawasilishwa tena kwa Kamishna, kwa ajili ya kuthibitisha kuwa maendeleo ya malezi ya kambo ni mazuri, hakuna changamoto hivyo, kibali cha kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya Kuasili mtoto huyo kitatolewa.

Hakuna malipo yoyote epuka ulaghai wa wasio waadilifu.
Mama nakupenda sana kwa kazi yako!

Mungu akutumie kwa njia hii na zaidi!
 
mheshimiwa hii kwa Tanzania yetu bado sana
 
Ninaye mtoto ambaye nimekuwa nikimlea kwa hiari yapata miaka 6 sasa, wazazi wake wote wapo ila walitengana mapema sana.... baba wa mtoto ndiye alikuwa rafiki yangu.

Baada ya kutengana kwao, baba hakutaka kuhusika na malezi kwa namna yoyote licha ya ushauri wangu kama rafiki..... mwisho mama mtoto akaniomba mimi nimsaidie malezi kwa kuishi na mtoto na kumsomesha.

Kuna nyakati kadhaa nimeshuhudia majina ya mtoto kwenye daftari zake akibadili na kuandika jina langu, ile kuulizia kumbe mama mtoto pia anajua na ameridhia.... kitu ambacho nimekipinga kwa kuwa nilihisi pengine itakuja kuleta shida mbeleni.

Kuna nyakati natamani kufanya hivyo ili kumwezesha mtoto kuwa mnufaika wa BIMA ya AFYA, ushauri niliopewa ni huu wa kumuasili ila bado sijafikia maamuzi..... sababu sijakubali kupora haki ya mzazi wake ambaye ni rafiki yangu japo hajali lolote ila huwezi kujua ya kesho.

Je, naweza kumuasili mtoto kisheria ili aweze kupata hizi 'benefits' lakini akabakia na majina yake?
 
Hongera sana kwa utu na upendo, unaweza kupata ushauri wa kitaalamu zaidi kwenye hizo namba. Ila ukipenda unaweza kunitumia ujumbe kwenye simu yangu nikuunganishe na Kamishna wa Ustawi moja kwa moja kwa elimu zaidi. Ila kuasili Nina mashaka, unaweza kuangukia kundi la malezi yale kwa sasa yanajulikana kama kambo, kisheria.
 
Back
Top Bottom