Mwaka jana spending cap kwa mgombea Urais ilikuwa bil 2. Sheria ya Kikwete, mwaka 2010,
CAP 278.
CCM wakaitisha fund raising event yenye malengo ya kukusanya bilioni 100.
Siku moja kabla ya fund raiser waandishi wakamuuliza Katibu Mkuu Nchimbi, hapo vipi, imekaaje kisheria hiyo ?
Emannuel Nchimbi akajibu akasema si kazi ya CCM ku enforce sheria za matumizi ya hela kwenye kampeni.
Kesho yake watu wakaja Mlimani City, wakamwaga bilioni kumi kumi!
Ili kulainisha mapito machafu ya biashara zako.
Halafu unatembea na kanzu nyeupe umekunja mikono kama mtakatifu!
Unashuka kwenye Rolls Royce. Limepita njia za vumbi. Viongozi corrupt uliowasapoti wamehujumu mradi wa barabara. Wewe unaona ni utu huo ?