GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Mwandishi maarufu wa vitabu, Robert T. Kiyosaki, kaandika kuwa mahali sahihi pa somo la mafanikio kufundishwa ni nyumbani. Kwa msingi huo, makuzi ya mtoto yatakuja kumwathiri si yeye peke yake tu, bali pia familia yake, Jamii yake na Taifa lake kwa ujumla.
Je! Malezi yetu ya Kitanzania yanamuandaa mtoto kuja kuwa mtu mwenye mafanikio kibinafsi na katika nafasi atakazozishika kwenye Jamii au Serikalini?
Ikiwa maisha ya utotoni ni kama msingi wa maisha ya utu uzima, namna watoto wa sasa wanavyolelewa kunatia matumaini kuwa kesho Taifa litakuwa na watu "potential?"
Kumbuka, watu wazima walio kwenye nafasi mbalimbali leo Serikalini, kwenye dini, Jamii, biashara, taaluma, n.k. ni watoto wa "Jana".
Ukiangalia Mataifa yaliyoendelea, na hapa, walengwa wakuu ni "Wazungu ", ingawa hawana ngozi ngumu na zinazostahilimili mazingira mbalimbali kama ngozi zetu, ni wazi kuwa fikra zao zimechochea sana maendeleo ya nchi zao.
Wanajulikana kuwa ni:
1. Wazalendo sana kwa nchi zao
2. Ni wajasiri hivyo hupenda kujaribu mambo mpya hata kama yanaonekana ni hatari.
3. Wabunifu
4. Wanajiamini
5. Watu waliozoeshwa kujitegemea tokea wakiwa wadogo
6. Hujiwekea malengo ya maisha mapema sana tokea wakiwa watoto wadogo
7. Huzoeshwa tabia ya usomaji vitabu tokea wakiwa wadogo sana.
Kupitia malezi ya "sasa" ya watoto wa Watanzania wanaoishi Tanzania, unaionaje Tanzania ya "kesho?"