Unaishi vipi na jirani anayependa dezo na kuombaomba?

Ujirani mgumu sana, hasa kama unatumia akili zako sawasawa.

Ngoja nikupe hii leo, mwambie simu huwa unachajia kazini hata kama anakua ni kweli una chaja nyingine.

Ila kama ni aina ya jirani anayenijia akilini mwangu, dawa yake ndogo sana. Ustaarabu mwingi ni utumwa kwa jamii za sasa.
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] itakuwa yeye ndiye anaipasi pasi
 
Haa haa kuna watu mmepinda
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
Acha roho mbaya wewe.. kwani kwenye katiba si imeandikwa Tanzania ni nchi ya kijamaa? Sasa wewe huo ubinafsi utakuwa raia wa nchi gani wewe?
 
Wewe na yeye ni jinsia mbili tofauti? If yes jiongeze mkuu!
 

[emoji1436][emoji1436][emoji1436][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu haya maisha ya kuomba omba hakuna anaye yapenda inafikia kipindi unapigika haswaa unakosa hata pesa ya kununua mboga,

Wavumilie tu ndugu yangu maisha yanabana sana
Hujakaa na mgogo wewe,ana kazi nzuri tu lkn ataomba omba kila kitu from chaji,chumvi,nyanya,tomato sauce et
Huo ni ujinga unamuambia huna, mtu anayefaa kusaidiwa ni mwenye kipato cha chini
 
Kuna watu nafikiri hiyo iko damuni. Hivyo wachukulie tu hivyo hivyo ukiona its too much mute.
 
Nakwambia hivi wanapenda sana tu,Kama wengine wanakufa na Tai zao shingoni kwanini wao wajifanye omba omba?
 

Dah Mzee mimi nilipata Jirani isee ni zaidi ya Omba omba kila kitu anaomba as if ndo uliyemleta mjini anaomba kuanzia chakula, pasi, charger, sabuni, chai , mafuta mara nikopeshe hela dah nilimchoma kwa kweli ikafika stage hata cm yake sipokei cz nimemchoka ukiona cm yake au kagonga mlango basi jua unaombwa hii tabia inanikera watu wa namna hii sijui hawanaga mshipa wa aibu isee kuomba ndo kitu siwezag
 
Hahahaha kabsa chief hakuna mazoea unakata kbsa mazoea nao wakikuzoea wataanza kuleta dharau
 
Kuna mpangaji mwenzangu hapa ana mume wake bodaboda hajamaliza hata wiki picha linaanza asubhi anamtoa mtoto wake aje kuomba uji au chai yaan yy hapiki sana sana ataenda kununua chai au uji, ukifika mchana hapiki chochote mnachopika anataka mumpatia na yy , yaan wiki tu tushamchoka namuonea huruma sana binti yao maana wakat mwingine hata hawajui amekula nn na Yuko wapi....

Wanaume tuangalie sana wanawake wa kuoa jamani.
 
Hapa ninavo type kuna jirani yangu yupo ndani kashika na remote zote za screen na king’amuzi yani imebidi nitoke tu nje nimwache lakini ikifika mida ya mechi za mpila naenda kumtoa..yan mtu ukimcheki mnaheshimiana lakini mambo yake ukiyatafakari unakuwa unajiuliza inamaana yeye haoni majirani zake wanaishi vipi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…