Natengwa na majirani sababu ya mmea, kuna kisa fulani nikikumbuka mpaka nacheka kuna siku nilikuwa naelekea dukani usiku kununua mkate maana kesho yake nilikuwa nawahi asubuhi sana kutoka.
Kuna mama fulani wa makamo alikuwa anaelekea njia moja na mimi ila yupo mbele yangu ndio anaenda nyumbani kwake sasa nikiongeza mwendo na yeye anaongeza mwendo nisimkaribie mpaka akakata sandals alizokuwa amevaa.
Kumsemesha namuona ana hofu kama anatetemeka na hasira, alibahatisha kuna toyo ilikuwa inapita akaichukua na kwenda nayo umbali haufiki hata nusu kilomita kesho yake nilikuja kusikia stori mtaani eti alinusurika kukabwa na wavuta bangi wa mtaani duh nikajua kumbe najulikana mtaani na na kuogopwa kabisa,
hamna mtu mwenye time na mimi wanajua ni mhuni tu anayepuliza mmea kila saa, na mimi nawaacha wanichukulie hivyo hivyo sitaki mazoea[emoji205]