Najua jirani ni ndugu wa karibu ila kuna mengine yamezidi.
Jirani alikuwa anakuja kuomba chaji nikaona sio kesi nimenunua nyingine nikamuachia atumie.
Bado basi yake imeharibika hana mpango wa kuitengeneza wala kununua nikaona sikesi usumbufu umezidi nichukue nyingine, sasa naona haajiongezi, chaji ile sijui imekuaje anakuja tena kugonga nimuwekee chaji, waungwana ujirani huu unafanyaje?
Mbona maisha hayo yalishapitwa sana na wakati jamani?
Maisha ya kuazimana nguo, viatu makoti, sijui chaja and the like ni ya kizamani!
Hayo ni mazoea ya ndani sana na ni dharau pia.
Halafu usije ukafikiri ni wema huo, kuzoea ku share vitu baadaye huleta majungu na kubweteka kwa utegemezi pamwe lawama.
Ujirani ni kusaidiana ndiyo, lakini kwa issue kubwa kubwa za dharula tu na si mambo ya kizembe yanayochukua muda kuyatanzua kama ya hilo la pasi na chaja.
Vitu ambavyo ni vya lazima katika maisha ya mtu ni muhimu kuvinunua na kuwa navyo.
Vinginevyo wakati mtu anajiandaa kuvinunua, avumilie, awe na subira na si lazima ku expose dhiki zake na kusumbua watu.
Tatizo usiyapodhibiti mazoea mapema hasa unapohamia sehemu kuanza maisha, baadaye mazoea hayo hugeuka na kuwa adha kubwa na kupoteza uhuru wako wa falagha.
Ukitaka kubadilika, weka kanuni kwa familia kwamba, kila jirani anapokuja kuazima kitu, atolewe nje kwa kuelezwa kwamba kitu hicho hakipo, kauli fupi na bila blah blah.
Halafu vitu vyote vinavyotamanisha kuazimwa vikae ndani ama store.
Akifanyiwa hivyo mara mbili hawezi kuendeleza mazoea yake kwako na ataacha.
Sent using
Jamii Forums mobile app