Unaishi vipi na jirani anayependa dezo na kuombaomba?

Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
😂
 
Bora nyie wanawaomba wenyewe jamani sisi tunaoshinda maofisini nyumnba inabaki na dada, akibaki dada wataombana watapeana na hodi zitagongwa.
NIkiwa nipo home husikii hodi wala kuombana.
Yaani kuna siku wameombana kisamvu 😂😂😂 ile nimefika kisamvu kimeingizwa na dada ndani.
Kumuuliza anasema nilikuwa na hamu nacho.
Nikamuuliza ulishindwa nini kuchuma ukatwanga na kupika ili tule nyumba nzima?je na wewe huwa unampa nini hadi yeye akupe kisamvu?na kama unampa hivi vitu ni vyako?

Mind you kisamvu nimepanda uwanjani kwangu, nazi na karanga zipo ndani.
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
🙄🙄🙄 Dahhh hii kiboko
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwrnye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
This is so Gangsta. 😅😅😅😅
 
Ni mwanamke au mwanaume? Nina sababu kuuliza swali hili.
 
Whaaaaaaat[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kama jinsia tofauti kuna charger ya aina nyingine anaitaka, shituka!!
 
Usikute huyo anakutaka tu ila anashindwa kukuomba gemu.
 
Dah kuna jirani mnyaturu asee huyu anaenda mlangoni kwa mwenzake anachukua viatu anaendea anapopajua yeye bila kuomba...mwenzake akitoka hakuna kiatu, anaomba gesi apikie/apashie, anaomba hela, anaomba chakula, anaomba yaaani kila kitu. Yaani yeye hata Bill ya maji halipi wala umeme. Anasubiri aombe na ajilize lize. Asee mashamba vijijini yapo kwanini msirudi huko mkalime kuliko mnavyoaibika mjini.
 
Ukitambua kwamba jirani ni sehemu ya maisha yako, hutahangaika.
 
Kuna Kisa kimoja cha mpangani ambaye mwenye nyumba wake alikuwa ni mwanamke mtu mzima kiasi kuingia tu yule mpangaji wa kiume, mama akaanza mwanangu utapaweza hapa mimi tabia yangu huwa natukana sana wapangaji ,yule mpangaji wa kiume akamwambia mama vyema kunijuulisha tabia yako na mm nina tabia mbaya vile vile huwa napenda kupiga wenye nyumba yule mama kimyaa ,jamaa kaishi pale mpaka kahama yule mama hakuwahi kumtukana hata siku moja.
 
@Nakadori umekuja kuntangaza mnyaturu wako huku mtandaoni? Au kisa nilikukula kimasihara![emoji3]

Joke, usichukie.
 
Kua makini mkuu , kuna siku linaweza tokea tukio baya mtaani kwenu hata kama hukufanya wewe , unaweza ukaja kuangushiwa msala ambao haukuhusu , jaribu kua mtu mwema , sio vizuri kuhusishwa kwenye vitu vya hovyo
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mpe ujumbe kuwa hupendelei tabia yake hiyo kwa njia ya indirect... Mwekee chaji akiondoka zima switch akija kuchukua simu haijajaa ..ikitokea hivyo mara tatu harudi
Ukimuendekeza atakuja kuomba mpaka mboga na siku akiwa na wageni atakuomba pa kulala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…