Unaishi vipi na jirani anayependa dezo na kuombaomba?

Mvumilie tu jirani ndio ndugu yako wa karibu hasa ukiwa uswahilini😂!

Kero ikizidi kuna Apartment Masaki hapa, nitafute nikupeleke kwa mwenyewe.
 
Akiomba mpe fake atajifunza
 
Mzee wa Shada😂 unakula sana dawa!
 
Nakataa ndugu, mtu ambae kwa mwezi anaingiza 500,000tsh anashindwa chaji ya 10,000? Kitu anachotumia mara nyingi?
Aaaaaaaa....umenikumbusha mbali sana nilikuwaga na jirani yangu yeye n mwalimu wa secondary.....alikuwa anaomba kiberiti mpaka perfume.
 
Ni kuwa bize na kazi ili asikukute Mara kwa Mara nyumbani!
 
maisha mepesi sana haya hasa ukijifunza kupuuza mambo,yaani kuwa mzungu tu.

unawezamkoromea huyo jamaa,akakuogopa kabisa mpaka siku umeanguka akaendelea kuogopa hata kukusogelea[emoji38][emoji38]
 
Aaaaaaaa....umenikumbusha mbali sana nilikuwaga na jirani yangu yeye n mwalimu wa secondary.....alikuwa anaomba kiberiti mpaka perfume.
Fikiria mtu mwenye mentality kama hiyo, yani ni kero sana
 
Mpe ujumbe kuwa hupendelei tabia yake hiyo kwa njia ya indirect... Mwekee chaji akiondoka zima switch akija kuchukua simu haijajaa ..ikitokea hivyo mara tatu harudi
Ukimuendekeza atakuja kuomba mpaka mboga na siku akiwa na wageni atakuomba pa kulala
Mkuu nitajiribu lakini naona kama hana mshipa wa aibu vile, siku unamuonesha kabisa umekasirika ila bado anarudi tena
 
Mimi jirani zangu tunaombana mbogamboga kwenye vibustani vyetu. Kama nimepanda mbogamboga hizi yeye hajapanda akiwa ana hamu nazo anakuja kuomba na mimi nikiwa na hamu na za mwenzangu namuomba.
Lakin sio kuombana vitu vingine.
Mi nataka nije niombe mboga mboga za mwilini zile jirani! Tuendelee na moyo wa mshikamano tu
 
Kuna mmoja alikuja kuazima pasi akaunguza waya nikakausha bahati nzuri nilikuanayo nyingine ambayo niliinunua nikiwa kwenye safari moja hivi, so kila akija kuomba nampa ile mbovu na sijui anaitumiaje!? Maana haipeleki moto
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukiweza kumsaidia jirani msaidie, kama huna uwezo au nafasi mueleze wazi na siyo kuja kumsimanga JF.

Unachopaswa kuelewa kila binadamu ana umuhimu wake hata anayezoa takataka ndio anakuokowa wewe nyumbani kwako pasinuke uvundo.

Tujifunze kuwaangalia wenzetu in positive way.

Kuna jamaa alipata tatizo kazini akajikuta yupo jela, kule lupango akakutana na mpiga debe wa daladala mtoto wa mtaani kazinguwa bararbarani wskamtia Segerea.

Baada ya yule jamaa kibosile wa mtaani kufika jela aliishi maisha salama na ya amani kupitia yule mpiga debe choka mbaya na akapewa na cheo gerezani kwa heshima tu.

Jamaa tangu ametoka jela alibadirisha mtazamo wake namna ya kuishi na binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…