Unaishi vipi na mpenzi wako mwenye asili ya udokozi?

Unaishi vipi na mpenzi wako mwenye asili ya udokozi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kuna huyu mpenzi wangu nashindwa kumuelewa, amekuwa na tabia ya udokozi udokozi wa hela.

Yeye haombi, akiona kuna laki atanivizia nikiwa nimelewa, anachomoa kama arobaini hivi anakaa kimya; huku akijua labda mimi nimepoteza kumbu kumbu.

Nikiuliza, mbona hapa hela imepungua; anasema labda sikuhesabu vizuri kabla.

Tabia hii, imekua ikijirudia; hii ni mara ya pili.

Natamani kumpiga chini, ila ndio hivyo tena ana kitambi.

Kumuambia kuwa yeye ndio amebeba, najua atajisikia vibaya ingawa ndio ukweli wenyewe.

Nataka nije nipige mkwara kwa kumuambia, nataka nisome albadiri kwa yule anayedokoa dokoa visalio vyangu apate madhara, ili nimsikie atasemaje.

Wakuu mna maoni gani?​
 
Mwambie baby wangu,,tupo wawili tu hapa,kuna hela huwa zinapotea,sitaki kuamini kuwa una tabia hii ila huenda una mahitaji unataka kuyasolve unaona aibu kuniambia

Just tell me baby wangu usiwe na hofu,hakika wewe ni mwanamke mrembo sana kufanya mambo kama haya,,,love you

Akikuibia tena nitag
 
Back
Top Bottom