Unaishi vipi na mpenzi wako mwenye asili ya udokozi?

Kuna huyu mpenzi wangu nashindwa kumuelewa, amekuwa na tabia ya udokozi udokozi wa hela.

Yeye haombi, akiona kuna laki atanivizia nikiwa nimelewa, anachomoa kama arobaini hivi anakaa kimya; huku akijua labda mimi nimepoteza kumbu kumbu.

Nikiuliza, mbona hapa hela imepungua; anasema labda sikuhesabu vizuri kabla.

Tabia hii, imekua ikijirudia; hii ni mara ya pili.

Natamani kumpiga chini, ila ndio hivyo tena ana kitambi.

Kumuambia kuwa yeye ndio amebeba, najua atajisikia vibaya ingawa ndio ukweli wenyewe.

Nataka nije nipige mkwara kwa kumuambia, nataka nisome albadiri kwa yule anayedokoa dokoa visalio vyangu apate madhara, ili nimsikie atasemaje.

Wakuu mna maoni gani?​
Labda pesa unazompa hazimtoshi.
 
Jiepushie matatizo ya baadae kwa kumuacha!
 
Mwambie ukweli tu....labda hiyo tabia amekuwa nayo muda mrefu sasa kupitia wewe anaweza kujirekebisha
Kuna wengine walikuwa walevi,wakaacha kutokana na hekima za wapenzi wao...sembuse hiyo
Nahisi anaweza kujisikia vibaya; ingawa mpaka sasa sijampigia simu naye pia hajanitafuta
 
Back
Top Bottom