Unaishi vipi na mpenzi wako mwenye asili ya udokozi?

Mimi usipokuwa kuwa unanitunza nakuwa kuwa mdokozi . Kweli ila ukinipenda nakunijali siwi mdokozi hata uwe umeacha ml 90 juu ya kitanda ninyime uone .
 
Kuleta mambo ya mapungufu ya mkeo ni kutoa siri za chumbani na kuziweka hadharani.

Ungelikuwa umepitia chuo cha jando usingelithubutu kutoka kadamnasini namna hii na kuongelea madhaifu ya mkeo wa ndoa.

Unavyofanya kijana sivyo, jirekebishe.
 
Mwambie ukweli tu....labda hiyo tabia amekuwa nayo muda mrefu sasa kupitia wewe anaweza kujirekebisha
Kuna wengine walikuwa walevi,wakaacha kutokana na hekima za wapenzi wao...sembuse hiyo
Baada ya kumuambia ukweli, akasema bora tuachane. Nami nikapigia mstari hapo hapo.
 
Kuleta mambo ya mapungufu ya mkeo ni kutoa siri za chumbani na kuziweka hadharani.

Ungelikuwa umepitia chuo cha jando usingelithubutu kutoka kadamnasini namna hii na kuongelea kashsifu ya mkeo wa ndoa.

Unavyofanya kijana sivyo, jirekebishe.
Ndio maana wanaume tunakufa mapema kwa sababu ya kubeba vitu kwenye vifua vyetu visivyokuwa na tija, waswahili wanasema, ongea tapika nyongo mwili ukae sawa.
 
Ndio maana wanaume tunakufa mapema kwa sababu ya kubeba vitu kwenye vifua vyetu visivyokuwa na tija, waswahili wanasema, ongea tapika nyongo mwili ukae sawa.
Kwa mkeo unarekebisha mwenyewe bhana.

Kuongelea jambo lolote ni afya kweli, lakini yakupasa uongee kwake ama uongee naye dhahiri ili arekebishe mapungufu yake hayo.

Sasa kila kero za mkeo utatoka hadharani kuziongea eti kwa sababu tu unatoa nyongo!

Mke ni 'mwili mmoja' na wewe, hivyo mapungufu yake ni mapungufu yako.

Kutoa dosari yoyote ya mkeo kwa watu ni kuanika dosari zako mwenyewe pia, yaani unajichoresha na kuwapa mahasimu wenu njia ya kuanzia kuwatendea mabaya kwa maneno ama kwa vitendo.

Ndicho nilichomaanisha.
 
Huyu ni mchepuko, mbaya zaidi anakataan na kukimbilia tuachane
 
Huyu ni mchepuko, mbaya zaidi anakataan na kukimbilia tuachane
Nilidhani ni mkeo wa ndoa ndiyo nikaongea nilichokiongea.

Mchepuko hana haki zozote za kisheria kwako.

Angelikuwa na nidhamu, angelitumia mahusiano hayo kama ni fursa ya 'future' yake.

Lakini sikio la kufa...
Msipotezeane muda na kibaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…