Unaishi vipi na mwanaume asiyepokea ushauri wa mwenza/ watu wengine?

Unaishi vipi na mwanaume asiyepokea ushauri wa mwenza/ watu wengine?

Hellow JF Members,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba maoni ya wadau. Unakuta mwenza ni mgumu sanaa kupokea ushauri hata wa kawaida tu na pale mambo yanapomuendea kombo juu ya jambo ulilomshauri anakurudia na anataka mshiriki wote kutatua.

Mfano anaweza fanya maamuzi ya kununua kitu fulani ukamwambia may b hapo siyo pazurii au hicho kitu unachotaka kununua kwa sasa hakina uhitaji mkubwa coz tuna mahitaji haya na hayaa ya msingi zaidii ni anakua mkaidi na kununua then kikiharibika anataka uchangie katika matengenezo nk.

Mfano mwingine mnaweza mkawa na ujenzi A unaendelea ghafla akaanzisha ujenzi B unamshauri kuwa hiyo pesa ya ujenzi B n heri tukamalizie kwanza ujenzi A then ndo uanzane na project B but atakaza fuvu ataenda anza ujenzi B mara paap pesa zinakataa hamna kitu ambacho kimekamilika as angemalizia ujenzi A basi hata mngepangisha then pesa ambazo zingepatikana hapo kutoka A zingeanza project B.yaan mifano ni mingi sanaaa sijui ni anakuwa na utemi ndani yake sielewi.

Naomba ushauri unadeal vipi na mtu wa tabia za mfanano huo??
Na imekuaje mwanamama wewe kujiita mkushi?
 
Kwanza ujiulize, Je, ni kwa nini hapokei ushauri wako????Je, Ushauri wako unaompatia ni mzuri na kweli una tija???? Je, huo ushauri wako unaompatia ni 'Constructive' au 'Destructive'??
Isije ikawa ushauri wako unaotoa ndio chanzo cha tatizoT
Kwanza ujiulize, Je, ni kwa nini hapokei ushauri wako????Je, Ushauri wako unaompatia ni mzuri na kweli una tija???? Je, huo ushauri wako unaompatia ni 'Constructive' au 'Destructive'??
Isije ikawa ushauri wako unaotoa ndio chanzo cha tatizo
Sasa ushauri wangu unakuaje chanzo cha tatizo na hauchukui?
 
Baadhi yetu sisi binadamu tunayo matatizo ya kukosa utulivu hasa tupatapo pesa /hela za mboga. Badala ya kutuliza akili tunakuwa na papara na kiherehere kwa kujiaminisha kwamba pesa ni Kila kitu, zikikata tu....ngebe zote kwishaaa

Huyo usimkatie tamaa endelea kutimiza wajibu wako kwa kumpa ushauri pengine ipo siku atabadilika
Kama ulikuwepo ni kweli kabisa,ngoja niendelee kupambana may b one day nitapata majibu chanya.
 
Kuna baadhi ya watu hawashauriki hata umpige panga, ushauri wako unapoteza bure.
Mmojawapo ni mimi nabeba risk ya kufanya maamuzi binafsi sihitaji ushauri na yakiharibika nitajua mwenyewe ila siwezi enda sumbua mtu kwa nilichoharibu, nitachora nianze moja.
Wewe upo vizuri,kwasababu matokeo unayabeba mwenyewe.
 
Ukiona hakusikilizi basi hilo jambo lifanye wewe. Kama project A kaiacha kaenda project B, basi wewe chukua jukumu la kuendeleza hiyo project A.

Kama kanunua kitu ambacho hakina umuhimu, basi wewe toa pesa yako nunua kile ulichomshauri. Akiona unachukua maamuzi, basi atakuja muungane.
 
Hujawahi kukutana na watu wasioshaurika. Na kama atakubali kufata ushauri wako ikitokea tatizo lolote lawama zinakuja kwako. Ni watu wagumu sana kudeal nao..
Mkuu hata wewe inaonekana ni aina ya watu kama mleta mada, mnapanick ushauri wenu usipotekelezwa na yakatokea maafa.

Badala yake mnalaumu na kulazimisha next time fata ushauri wangu. Kwa mwanaume hiyo ni ngumu hasa kama yeye ndo mwenye fuba.
 
Mkuu hata wewe inaonekana ni aina ya watu kama mleta mada, mnapanick ushauri wenu usipotekelezwa na yakatokea maafa.

Badala yake mnalaumu na kulazimisha next time fata ushauri wangu. Kwa mwanaume hiyo ni ngumu hasa kama yeye ndo mwenye fuba.
Mimi sipanick mtu asipotekeleza ushauri wangu...kwanza nimeshaacha kutoa ushauri maana haisaidii...
Namwacha afanye atakavyo..ikitokea kachemka namwambia neno moja tu nimemaliza...POLE.

Akiomba ushauri namwambia fanya tu vile unavyoona ni sawa. Hakuna haja ya kupanic
 
Usifosi ushauri wako utumike kwenye pesa ya mtu mwingine, we kama umeolewa base kwenye duties zako zinazokuhusu kama kufua, kupika na usafi hayo mengine ni juu ya mme wako akiamua akushirikishe ni sawa asipo amua kukushirikisha ni sawa pia kwasababu Yeye ndio Bosi kwenye familia yenu anajua nini atafanya chakula kipatikane na wewe kama mke wake upendeze.
 
Sasa kwa style hiii mkuu unakuta malengo ya familia yanachelewa au hayafikiwi kutokana na ukaidi/kutokuwa na masikilizano ya mtu mmoja yanagharimu familia nzima kwa ujumla mkubwa.
Wewe ulipoanza kufanya Plan zako yeye mbona hakupinga??? Wanawake huwa mna changamotoo sanaa unataka ununue kiwanja kimyakimyaa au ufanye ujenzi kiwanja cha urithi bila kiomba ushaurii ila mwenzio akianza kufanya jambo lake unaona hayupo sahihiii..
 
Back
Top Bottom