Unaishije na rafiki/mpenzi ambaye hawazi kabisa kuhusu maendeleo?

Unaishije na rafiki/mpenzi ambaye hawazi kabisa kuhusu maendeleo?

CONTRARIAN

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2023
Posts
982
Reaction score
3,137
Nazungumzia mtu ambaye kwa kiasi kikubwa mpo karibu sana..

Yaani kama ni mpenzi yeye anataka udaku, kudinyana, romance...

Rafiki naye, stori ni za Mahusiano tuu, n.k

Kwa ufupi hakupi challenge yoyote ile.., kuna mda unahitaji kua peke yako ili angalau uwaze nje ya boksi,

Ukimshirikisha jambo/mchongo anaitika ila soon analipotezea.., yeye ni wa mshahara.., kuna michongo mingi sana anapata ila anaipotezea,

Kimaendeleo angekua mbali mnoo kunizidi, kwa ufupi ana bahati, kuna mda ukimuuliza kwa nini upo hivi? Anakua kama anachukia, hapo nashindwa kuendelea, nishamuunganishaga na dili moja la maana na uhakika baadae akalitema, nikampa lijama flani lisilo na shukrani.

Unakaa unajiuliza hivi huyu kuna hata dk inaenda anawaza future yake?, maana yake achilia mbali tuu kutokushirikisha,
Ni mtu ambaye Kwa ufupi unamjua IN and OUT hana anachokifanya....

Ikiwa ni wewe utafanyaje? Kwa upande mwingine ni mtu poa sanaa, very friendly na supportive.
Ila natamani abadilike.
 
MTU mwenye mshahara Ni ngumu Sana kumshawishi kufanya Kazi nyingine [emoji23],hasa kama hio Kazi inatumia nguvu nyingi kuzid anayofanya hata kama unapesa nyingi ...utasikia anasema maisha Ni haya haya ...madili ya hivo tupe Sisi
 
Ningepata rafiki kama wewe ningekiwa mbali sana,najuta kupoteza miaka yangu kwenye kazi za kuajiriwa
 
FB_IMG_17111311639621872.jpg
 
Hivi unajua kujihusisha sana na mambo ya mtu kunaleta stress??? Mtu anaeweza kua mme/mke/ndugu au rafiki....unataka stress??? Zinakusaidia?!

Mambo yake muachie mwenyewe, keep silence, stay positive, fanya mambo yako.
Atakama ni mwenza wako?
 
Ila sikujua kama wanawake wanabadirika sana kwenye ndoa,yaliyonikuta yanasikitisha.Nibaada yakipato changu kupungua,nilikuwa mwajiliwa company ya private wife yy yupo serikalini.
 
Sema watu wengi dizain hio kwa experience wanakuaga na Discipline ya pesa sana.
Hii ni kwelii, Humuambii kitu kuhusu kuweka pesa ya akiba bank,

Mimi Pesa siiweki, inazunguka/wekeza...
Kwahio mda mwingi sina cash, nikipata dharura ya chap yeye ndio wa kwanza...
 
Hii ni kwelii, Humuambii kitu kuhusu kuweka pesa ya akiba bank,

Mimi Pesa siiweki, inazunguka/wekeza...
Kwahio mda mwingi sina cash, nikipata dharura ya chap yeye ndio wa kwanza...
Sasa huoni hio ndio ecosystem, kutokua kwake na mishe somehow ni advantage kwako, huyo mtumie kwenye backup, hapo wote mtakua mnasaidiana,

Wewe unaonesha risk taker, sasa mke risks takers, mme risks takers, Risk iki take part si mtakimbiana?

BTW huko huko mwambie Aweke hata fixed account/UTT etc.

Mwisho, Acha kuzunguka, OA huyo ni mke.
 
Wqkati fulani nikiwa na mtu mmoja aliyekuwa rafiki wa karibu sana alikuwa na tabia ambayo tulikuwa tunashindwana..ni mtu wa kufanya maendeleo sana lakini si timilifu. ..project zake zilikuwq hasitimii anahamia nyingine ..anaweza jenga nyumba hadi kupaua anaacha akipata kiwanja mahali ananunua anajenga tena anaacha pagale anaacha anahamia project nyingine anajenga anaweka mtu anakaa mle ndani (aliwahi kaa mtu bure for more than 5 yrs nyumba imekamilika kilakitu isipokuwa milango 2 tu ya chooni mastre na public toilet )ilibaki maboresho kidogo nyumba irudishe pesa still ikatelekezwa hivo..mnaweza plan vizuri this time fanya hiki na hiki unastukia kaibuka na kingine tena bila kushirikishwa..so ilifika hatua nkamuacha aongozwe na maamuzi anayoona ni sahihi japo hata akikushirisha unaitikia tu bila kutia neno maana hata ukishauri hakuna kinachotekelezeka na yuko hivo mpaka leo nainconplete project zake japo sipo nae karibu kama mwanzo..kuna watu vichwq ngumu nyie khaa
 
Hili ni tatizo na no sawa na kupanda mbegu juu ya mwamba
 
Hii ni kwelii, Humuambii kitu kuhusu kuweka pesa ya akiba bank,

Mimi Pesa siiweki, inazunguka/wekeza...
Kwahio mda mwingi sina cash, nikipata dharura ya chap yeye ndio wa kwanza...
Mambo ya utafutaji ni kipaji sio kila mtu anacho mkuu.
Hata hivyo kama ana nidhamu ya pesa na mazuri yake mengine inatosha
 
Back
Top Bottom