Unaishije na rafiki/mpenzi ambaye hawazi kabisa kuhusu maendeleo?

Unaishije na rafiki/mpenzi ambaye hawazi kabisa kuhusu maendeleo?

Nazungumzia mtu ambaye kwa kiasi kikubwa mpo karibu sana..

Yaani kama ni mpenzi yeye anataka udaku, kudinyana, romance...

Rafiki naye, stori ni za Mahusiano tuu, n.k

Kwa ufupi hakupi challenge yoyote ile.., kuna mda unahitaji kua peke yako ili angalau uwaze nje ya boksi,

Ukimshirikisha jambo/mchongo anaitika ila soon analipotezea.., yeye ni wa mshahara.., kuna michongo mingi sana anapata ila anaipotezea,

Kimaendeleo angekua mbali mnoo kunizidi, kwa ufupi ana bahati, kuna mda ukimuuliza kwa nini upo hivi? Anakua kama anachukia, hapo nashindwa kuendelea, nishamuunganishaga na dili moja la maana na uhakika baadae akalitema, nikampa lijama flani lisilo na shukrani.

Unakaa unajiuliza hivi huyu kuna hata dk inaenda anawaza future yake?, maana yake achilia mbali tuu kutokushirikisha,
Ni mtu ambaye Kwa ufupi unamjua IN and OUT hana anachokifanya....

Ikiwa ni wewe utafanyaje? Kwa upande mwingine ni mtu poa sanaa, very friendly na supportive.
Ila natamani abadilike.
Mtu wa hivyo wa nini sasa mm namuacha.
 
Hivi unajua kujihusisha sana na mambo ya mtu kunaleta stress??? Mtu anaweza kua mme/mke/ndugu au rafiki....unataka stress??? Zinakusaidia?!

Mambo yake muachie mwenyewe, keep silence, stay positive, fanya mambo yako.
Kabisaaa!!
 
Unakuta mke au mume hafikirii kabisa maisha ya baadaye, na wengine hata maisha aliyonayo kwa sasa hajui yanaendeshwaje kwa sababu siyo yeye ndiyo mtafutaji. Hana motivation, hana hata japo kuchangia mawazo ya kuboresha maisha. Kwa wanawake kama hawa, yeye anachojua tu kujipodoa uso. Mvivu hata kazi za ndani hafanyi. Unakuta ukitoka kazini nyumba chafu. Hajui hata bills za ndani ni kiasi gani au zinalipwaje. Yaani ni shida tupu. Watu kama hawa ni mzigo haswa. Ila kwa kuwa umesha zaa naye, inabidi tu umkongoje hivo hivo, ila wewe kama mwanaume au mwanamke mwenye mwenza wa design, endelea tu kupigania maisha, na usisahau kufanya yako kujiandaa na maisha ya uzeeni, hata ikiwa ni kwa siri. Huyo mpuuzi uliyenaye abaki aendelee kufanya upuuzi wake usioleta maendeleo. Maisha haya!!! Usiombe yakukute una mwenza bogus!!
 
Back
Top Bottom