Unaishije na rafiki/mpenzi ambaye hawazi kabisa kuhusu maendeleo?

Mtu wa hivyo wa nini sasa mm namuacha.
 
Hivi unajua kujihusisha sana na mambo ya mtu kunaleta stress??? Mtu anaweza kua mme/mke/ndugu au rafiki....unataka stress??? Zinakusaidia?!

Mambo yake muachie mwenyewe, keep silence, stay positive, fanya mambo yako.
Kabisaaa!!
 
Unakuta mke au mume hafikirii kabisa maisha ya baadaye, na wengine hata maisha aliyonayo kwa sasa hajui yanaendeshwaje kwa sababu siyo yeye ndiyo mtafutaji. Hana motivation, hana hata japo kuchangia mawazo ya kuboresha maisha. Kwa wanawake kama hawa, yeye anachojua tu kujipodoa uso. Mvivu hata kazi za ndani hafanyi. Unakuta ukitoka kazini nyumba chafu. Hajui hata bills za ndani ni kiasi gani au zinalipwaje. Yaani ni shida tupu. Watu kama hawa ni mzigo haswa. Ila kwa kuwa umesha zaa naye, inabidi tu umkongoje hivo hivo, ila wewe kama mwanaume au mwanamke mwenye mwenza wa design, endelea tu kupigania maisha, na usisahau kufanya yako kujiandaa na maisha ya uzeeni, hata ikiwa ni kwa siri. Huyo mpuuzi uliyenaye abaki aendelee kufanya upuuzi wake usioleta maendeleo. Maisha haya!!! Usiombe yakukute una mwenza bogus!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…