Unajiandaa kuangalia fainali ya kukumbukwa ukiwa wapi?

Unajiandaa kuangalia fainali ya kukumbukwa ukiwa wapi?

Wife simba nini mwanawane...hapo unaomba simba afunge magoli tuu ili baadae na weye ukafunge magoli kwenye uwanja mdogo

Sio mpenzi wa mpira. Ila matangazo ya azam kila siku amekua na hamu ya kuangalia hii mechi
 
Leo ni siku muhimu na maalum sana kwenye ulimwengu wa soka Tanganyika pale Mnyama Simba mwakilishi pekee wa kimataifa Tanganyika... Atakaposhuka dimbani huko Morroco kumenyana kwenye fainali za CAF

Ni siku maalum sana kwa SIMBA kwakuwa ilifanikiwa kufika hatua hii miaka 30 iliyopita
Ni siku maalum pia kwakuwa mpaka kufika hapo ametoka mbali sana

Basi itengenezee umaalum wake kwakuwa huna hakika ya kuja kuona fainali nyingine.. Ifanye siku ya leo kuwa tukio la kipekee sana..

Mimi nimeshatua Bukoba hapa tangu jana lakini final destination ni hapo kwa M7 Kampala kiwanja maarufu cha PLAN B mtaa wa Mengo
Kwakuwa SIMBA anaenda kuushangaza ulimwengu wa soka..basi siku ya leo ifanye maalum sana kwa wivu mkubwa kabisa
Wabongo mlioko Kampala see you baadae PLAN B .. Tutatambuana kwa mavazi na lafudhi
Mungu ibariki SIMBA❤💕❤💕
Mechi saa ngapi
 
Niko Mtwara, shughuli zimenibana ila ikifika mida ya mechi, ntaoga, nivae kijora kisha nijongee kunakooneshwa mtanange wa Simba.

Nakunywa maji ya tangawizi kwa wingi kuweka koo na sauti sawa ili nipige ukunga wa kutosha kila goli litapoingia....😊.

Amsha amsha kama kawa, kama dawa...😅.

Sijui nimeanza kumiksi madesa au niko kwenye mstari eehehe.

Poa poa, midamida 😉.
🔥🔥🔥
🦁
 
Mlimani City.
Na wadau kibao wa 🦁, tukianikiza mayowe na kelele za kusapoti chama letu.

Hii tunabebaaaaa.
 
Back
Top Bottom