UNAJIMU: Sayari ya Mercury na Athari zake katika Maisha yetu

UNAJIMU: Sayari ya Mercury na Athari zake katika Maisha yetu

kichekoh

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2015
Posts
1,376
Reaction score
1,479
Kuanzia tarehe 26/07/2018 usiku saa 7 hadi tarehe 19/08/2018 sayari ya Mercury inakua inazidiwa kasi na Dunia hivyo sayari ya Mercury kuonekana kama inarudi nyuma lakini kiuhalisia inakua inakwenda katika mwendo wake wa kawaida.

Tukio kama hili kinajimu kinaitwa (Retrograde), na kwa sayari ya Mercury hufanya hivi Mara 3 hadi 4 ndani ya mwaka 1. Mercury huwa katika hali hiyo kwa muda wa siku 21 hadi 25.

TAFSIRI YAKE KINAJIMU.

Mercury inapokua katika hali hii huleta mkanganyiko katika masuala yote yanayohusu mawasiliano. Kuanzia mazungumzo ya kila siku, mikataba, kuuza na kununua, hati, makubaliano, safari, barua na mengine yanayofanana na hayo.

Mambo hayo niliyoyotaja hapo juu huwa katika mwendo wa kujikongoja tofauti na ilivyo kawaida. Kunakua na kuchelewa na changamoto nyingi sana katika masuala mengi yanayohusu mawasiliano.

Hivyo katika kipindi hiki si kizuri kufanya yafuatayo;

kusaini mkataba wowote muhimu, kuanzisha biashara mpya, hakikisha unapitia kwa umakini meseji tunazotuma na kuzipokea. Kuhama na kuhamia nyumba mpya. Mercury unapokua katika hali hii huwa inaleta utata katika mazungumzo ya kila siku. Mtu anaweza akakwambia hivi halafu unaemwambia akaelewa tofauti na ulivyokusudia. Kwa hiyo ni vizuri kuuliza mara mbili kama hujaelewa.

Hiki ni kipindi kizuri cha kufanya marekebisho vitu vyote vinavyohusiana na mawasiliano kama vile simu, computer, radio, Tv lakini sio muda wa kununua chochote kipya kinachohusiana na hiki. Pia ni muda wa kurudia kusoma upya barua, documents, na kupitia upya mikataba ambayo uliosaini hapo mwanzo. Kufanya hivi kutapelekea kugundua tatizo ambalo hukuligundua mwanzo.

Mwenye masikio na asikie......

Kwa Ushauri, Elimu etc.... Nicheki.
WhatsApp 0782 82 11 77.
 
Kusomewa nyota ni kujihusisha moja kwa moja na shetani,unakuwa chini ya himaya yake.
Ni bora kuwa mtumwa wa haki kuliko dhambi.
Yawezekana ukawa hujui unaongea kitu gani... Miaka ya nyuma na mimi nilikua fikra kama zako. Ila baada ya kuziacha huru fikra zangu kwa sasa nimepiga hatua kubwa sana.
 
Je kusafisha nyota kuna uhusisno na unajimu wa mercury?
 
Mkuu hii kitu haileti maana kabisa, it seems like Kiranga was right.
Najua huwezi kuelezea kwa namna isiyopingika nikwajinsi gani movement au tofauti ya kasi za sayari mbili iweze kuleta athari kwenye kusaini mikataba, mazungumzo ya kila siku, kuuza na kununua, makubaliano etc...

In short, this doesn't make any sense.
 
Kama haya mambo yangekuwa yanaeleweka kwa wepesi kama unavyodhani, basi kila mtu angekua mnajimu.

Hii elimu ni ngumu kuielewa kuliko unavyodhani.
 
Kama haya mambo yangekuwa yanaeleweka kwa wepesi kama unavyodhani, basi kila mtu angekua mnajimu.

Hii elimu ni ngumu kuielewa kuliko unavyodhani.
Mkuu kama kweli ni ngumu kama ambavyo unataka kuniaminisha, sasa nitajuaje kama kweli wewe unaijua.
 
Mkuu kama kweli ni ngumu kama ambavyo unataka kuniaminisha, sasa nitajuaje kama kweli wewe unaijua.
Kwa hiyo kila kitu kigumu hakijulikani?

Ninachotaka uelewe hapa, Kuusoma na kuuelewa unajimu sio kama kukanda chapati. Unatakiwa uwe zaidi ya serious kuimaster hii kitu.

Mi nimetumia miaka 3 lakini bado kuna watu sijawafikia.
 
Naimani kwa elimu yako ya miaka mitatu unaweza kuniondolea utata nilionao, ni kwa namna gani hiyo tofauti ya kasi za sayari inaweza kunizuia nisisaini mikataba ya muhimu,nisisome barua n.k
 
Naimani kwa elimu yako ya miaka mitatu unaweza kuniondolea utata nilionao, ni kwa namna gani hiyo tofauti ya kasi za sayari inaweza kunizuia nisisaini mikataba ya muhimu,nisisome barua n.k
Unajua kinacholeta utata kwenye elimu hii ya unajimu ni kuhusianisha yanayotokea angani na maisha yetu hapa duniani. Hapo ndio kwenye tatizo.

Hata hivyo umeuliza swali sana. Ni hivii, sayari inapokua katika hali kama hiyo (Retrograde) huwa inakua haipo katika hali yake ya kawaida (direct motion). Hivyo inakua kama imeweka pause kwa kipindi chote inachokua retrograde.

Inakua kama vile mtu ambaye kaamua kujipa likizo kwa muda. Mfanyakazi anapojipa likizo ina maana anafunga ofisi. Ofisi inapofungwa ina maana hakuna huduma.

Hicho ndicho inachofanya Mercury, inapumzika kwa muda takribani siku 21 hadi 25. Inakua ina slow down. Na hufanya hivyo mara 3 had 4 ndani ya mwaka 1.

Utata mwingine kati ya sisi wanajimu na nyinyi upo hapa, kwamba wanajimu huamini kwamba Mercury ndio msimamizi wa masuala yote yanayohusu mawasiliano na masuala yote niliyotaja kwenye mada yangu.

Sasa kama msimamizi wa hayo mambo yupo likizo je nani atayasimamia hayo mambo?

Jibu lake inabidi sisi tusubiri mpaka muda ofisi itakapofunguliwa. Lini? Tarehe 19 august. Kwa hiyo mambo yote yanayosimamiwa na mercury inabidi yaachwe kwa sasa.

Unajua kwa nini mercury anasimamia hayo mambo?? Elimu hiyo naitoa darasani kwangu sio hapa.

Nimetumia lugha nyepesi kwa sababu ili hata asiyejua nae ajifunze.

Swali jingine tafadhali.
 
ama kweli huo ni unajimu maana maana ulichokisema hakina mantinki yoyte ile kisayansi,
 
Kwa mawazo haya mleta uzi utakua umezidisha dozi ya kitu cha Arusha,how comes speed ya mercury iwe ina control uwezo wako wa kufikiri na kutoa maamuzi?
 
Back
Top Bottom