UNAJIMU: Sayari ya Mercury na Athari zake katika Maisha yetu

UNAJIMU: Sayari ya Mercury na Athari zake katika Maisha yetu

Nyuzi nyingine naachia wadanganyane tu.

Nawasoma naona ujinga kama vichekesho fulani kwamba dunia ya keo ya kutembea na internet kiganjani kwenye 4G network, bado watu wanaamini ujinga wa kijima.

Eti Mercury in retrograde inasababisha mkinzano kwenye mikataba.

What a load of bollocks.
Haahahahaaa dah we jamaa unanipa raha sana.
 
Nyuzi nyingine naachia wadanganyane tu.

Nawasoma naona ujinga kama vichekesho fulani kwamba dunia ya keo ya kutembea na internet kiganjani kwenye 4G network, bado watu wanaamini ujinga wa kijima.

Eti Mercury in retrograde inasababisha mkinzano kwenye mikataba.

What a load of bollocks.
Itabidi ubadili username, wakuite mtibuaji
 
Na mimi nina swali lako ManchoG , hivi kwa nini tabiri za kinajimu zina mapokeo tofauti ukilinganisha na tabiri zingine kama tabiri za hali ya hewa (weather forecast) ama tabiri za mahitaji (demand forecasts)

Sina utaalamu wa tabiri ya aina yeyote kati ya hizo hivyo sina la kuongeza/kuzungumzia

Kumbuka zote hizo ni tabiri, na watu wanachukulia kawaida. Kwa nini unajimu?

Labda kulingana na mafundisho waliyozoezwa mashuleni

Tumefundishwa toka tukiwa wachanga kuwa sayari ni magimba tu yaliyo angani

Na hatukudokezwa juu ya kuwa na uweza zaidi ya huo wa kutawala haiba zetu

Endelea kutupa darasa tukiwa na swali tutawasilisha
 
Sina utaalamu wa tabiri ya aina yeyote kati ya hizo hivyo sina la kuongeza/kuzungumzia

Labda kulingana na mafundisho waliyozoezwa mashuleni

Tumefundishwa toka tukiwa wachanga kuwa sayari ni magimba tu yaliyo angani

Na hatukudokezwa juu ya kuwa na uweza zaidi ya huo wa kutawala haiba zetu

Endelea kutupa darasa tukiwa na swali tutawasilisha
Sio kila elimu utaipata darasani, haya mambo mengine yakupasa ujiongeze.

Na kanuni ya kwanza ya kuelewa haya mambo ni kuiacha akili yako huru. Utajua mengi sana kuhusu huu ulimwengu.
 
Sio kila elimu utaipata darasani, haya mambo mengine yakupasa ujiongeze.

Na kanuni ya kwanza ya kuelewa haya mambo ni kuiacha akili yako huru. Utajua mengi sana kuhusu huu ulimwengu.
Thibitisha Mercury inavyoathiri mikataba duniani.
 
Kama naitwa mtibuaji kwa kutibua uongo, jina hilo litakuwa la heshima kubwa sana kwangu.

Thibitisha Mercury inavyoathiri mikataba duniani.
Mkuu hilo nishalijibu, anzia comment za mwanzo kabisa za huu Uzi...
 
Unajua kinacholeta utata kwenye elimu hii ya unajimu ni kuhusianisha yanayotokea angani na maisha yetu hapa duniani. Hapo ndio kwenye tatizo.

Hata hivyo umeuliza swali sana. Ni hivii, sayari inapokua katika hali kama hiyo (Retrograde) huwa inakua haipo katika hali yake ya kawaida (direct motion). Hivyo inakua kama imeweka pause kwa kipindi chote inachokua retrograde.

Inakua kama vile mtu ambaye kaamua kujipa likizo kwa muda. Mfanyakazi anapojipa likizo ina maana anafunga ofisi. Ofisi inapofungwa ina maana hakuna huduma.

Hicho ndicho inachofanya Mercury, inapumzika kwa muda takribani siku 21 hadi 25. Inakua ina slow down. Na hufanya hivyo mara 3 had 4 ndani ya mwaka 1.

Utata mwingine kati ya sisi wanajimu na nyinyi upo hapa, kwamba wanajimu huamini kwamba Mercury ndio msimamizi wa masuala yote yanayohusu mawasiliano na masuala yote niliyotaja kwenye mada yangu.

Sasa kama msimamizi wa hayo mambo yupo likizo je nani atayasimamia hayo mambo?

Jibu lake inabidi sisi tusubiri mpaka muda ofisi itakapofunguliwa. Lini? Tarehe 19 august. Kwa hiyo mambo yote yanayosimamiwa na mercury inabidi yaachwe kwa sasa.

Unajua kwa nini mercury anasimamia hayo mambo?? Elimu hiyo naitoa darasani kwangu sio hapa.

Nimetumia lugha nyepesi kwa sababu ili hata asiyejua nae ajifunze.

Swali jingine tafadhali.
Majibu yapo hapa...
 
Mkuu hilo nishalijibu, anzia comment za mwanzo kabisa za huu Uzi...
Nimesoma sijaona uthibitisho.

Comment gani hiyo isiyo na namba wala kiweza kunukulika?
 
Last edited:
Utata mwingine kati ya sisi wanajimu na nyinyi upo hapa, kwamba wanajimu huamini kwamba Mercury ndio msimamizi wa masuala yote yanayohusu mawasiliano na masuala yote niliyotaja kwenye mada yangu.

Sasa kama msimamizi wa hayo mambo yupo likizo je nani atayasimamia hayo mambo?

Hii ina ukakasi sana _Na kama tayari ni Imani ni tatizo
 
Comment namba 13 haijathibitisha jinsi Mercury inavyoathiri mikataba duniani.

Imethibitisha huwezi kuthibitisha.
Kwanza kubali kama hujaelewa, halafu kitu kingine mtu ambaye beginner kama wewe, unapotaka kuelewa kwa usiku mmoja unakua unashangaza.

Una safari ndefu sana kuyaelewa haya mambo. Nimeeleza just in brief. Kitu ambacho kitakupa shida sana mtu kama wewe ambaye huna msingi wowote.

Unaweza elewa masomo level ya form six ikiwa hujaanza hata form one? Utakua genius.
 
Zote hizi ni longolongo za kuficha ukweli kwamba huwezi kuthibitisha madai yako ya uongo.

Wewe ni muongo.

Unasema Mercury inaathiri mikataba duniani.

Uzi huu nimekutaka ithibitishe hilo.

Umeshindwa.

Kwa sababu ni uongo.
 
Zote hizi ni l9ngol9ngo za kuficha ukweli kwamba huwezi kuthibitisha madai yakobya uongo.

Wewe ni muongo.

Unasema Mercury inaathiri mikataba duniani.

Uzi huu nimekutaka ithibitishe hilo.

Umeshindwa.

Kwa sababu ni uongo.
Hujui unachotaka, nimekwambia soma comment namba 13. Unasema haitoshi, hayo mengine unayotaka niandike hapa yapo nje ya uwezo wako.
 
Hujui unachotaka, nimekwambia soma comment namba 13. Unasema haitoshi, hayo mengine unayotaka niandike hapa yapo nje ya uwezo wako.
Hakuna ulipothibitisha Mercury inavyoathiri mikataba duniani katika hiyo post namba 13.

Kama kuna sehemu umeonesha hili, nukuu hapa.

Unadanganya vitu na ukiambiwa umedanganya unazidi kudanganya kwa kusema umevielezea wakati hujavielezea.

Unaongeza uongo juu ya uongo.
 
Mercury ni ruler wa mambo yote yanayohusu mawasiliano, sasa inapokua ina transit retrograde ina express its energy inwardly more than outwardly.

Ni kama ina pause for some time. Sasa na mambo yote yanayohusu mercury ikiwemo mikataba nayo yanakua katika sluggish state.

That's why tunashauriwa na sisi tuachane na mambo yanayohusu mercury at all ikiwemo mikataba.

Usipoelewa na hapo ntaanza kupata mashaka na wewe.
 
Kuanzia tarehe 26/07/2018 usiku saa 7 hadi tarehe 19/08/2018 sayari ya Mercury inakua inazidiwa kasi na Dunia hivyo sayari ya Mercury kuonekana kama inarudi nyuma lakini kiuhalisia inakua inakwenda katika mwendo wake wa kawaida.

Tukio kama hili kinajimu kinaitwa (Retrograde), na kwa sayari ya Mercury hufanya hivi Mara 3 hadi 4 ndani ya mwaka 1. Mercury huwa katika hali hiyo kwa muda wa siku 21 hadi 25.

TAFSIRI YAKE KINAJIMU.

Mercury inapokua katika hali hii huleta mkanganyiko katika masuala yote yanayohusu mawasiliano. Kuanzia mazungumzo ya kila siku, mikataba, kuuza na kununua, hati, makubaliano, safari, barua na mengine yanayofanana na hayo.

Mambo hayo niliyoyotaja hapo juu huwa katika mwendo wa kujikongoja tofauti na ilivyo kawaida. Kunakua na kuchelewa na changamoto nyingi sana katika masuala mengi yanayohusu mawasiliano.

Hivyo katika kipindi hiki si kizuri kufanya yafuatayo;

kusaini mkataba wowote muhimu, kuanzisha biashara mpya, hakikisha unapitia kwa umakini meseji tunazotuma na kuzipokea. Kuhama na kuhamia nyumba mpya. Mercury unapokua katika hali hii huwa inaleta utata katika mazungumzo ya kila siku. Mtu anaweza akakwambia hivi halafu unaemwambia akaelewa tofauti na ulivyokusudia. Kwa hiyo ni vizuri kuuliza mara mbili kama hujaelewa.

Hiki ni kipindi kizuri cha kufanya marekebisho vitu vyote vinavyohusiana na mawasiliano kama vile simu, computer, radio, Tv lakini sio muda wa kununua chochote kipya kinachohusiana na hiki. Pia ni muda wa kurudia kusoma upya barua, documents, na kupitia upya mikataba ambayo uliosaini hapo mwanzo. Kufanya hivi kutapelekea kugundua tatizo ambalo hukuligundua mwanzo.

Mwenye masikio na asikie......

Kwa Ushauri, Elimu etc.... Nicheki.
WhatsApp 0782 82 11 77.

Haya Mambo yapo! Elimu ya Unajimu (Astrology) hii ipo tangu zamani sana!(Occultism) Kuna Watawala Maarufu sana Ulimwenguni hawaanzi jambo lolote lile bila kutafuta ushauri kutoka kwa Wanajimu(Waonaji) - Kwa Watu wa Imani ya Kikristo ambayo ninaifahamu - Unajimu ni DHAMBI! Wenzetu waislam wanasema NI SHIRKI!
Kwa wasio na KATAZO elimu hii wanaifuata sana! WANASIASA,WANAMUZIKI NA WASAKA BAHATI ZA MAISHA.
Kwa sisi wenye KATAZO Elimu hii sio Sahihi kuiendea!
Na sababu kubwa ni kwamba utaacha kumtegemea MUNGU na kutegemea Maarifa ya hawa wasoma Nyota.
Utaacha kujituma na Kutumia Akili yako na Kuwa tegemezi wa Mambo yasiyo na Uhakika kwa Asilimia 100%
Upo Ushahidi wa Jinsi maisha ya watu yalivyoharibika kwa kuendekeza Unajimu - Hawezi hata kujaribu fursa mpya kwa kuwa Mnajimu wako kasema tofauti.
Astrology is a disease, not a science... It is a tree under the shadow of which all sorts of superstitions thrive. ... Only fools and charlatans lend value to it. - MOSES MAIMONIDES
Asante.
 
Mercury ni ruler wa mambo yote yanayohusu mawasiliano, sasa inapokua ina transit retrograde ina express its energy inwardly more than outwardly.

Ni kama ina pause for some time. Sasa na mambo yote yanayohusu mercury ikiwemo mikataba nayo yanakua katika sluggish state.

That's why tunashauriwa na sisi tuachane na mambo yanayohusu mercury at all ikiwemo mikataba.

Usipoelewa na hapo ntaanza kupata mashaka na wewe.
Hujathibitisha. Umeandika tu.

Kama mimi ninavyoweza kuandika kwamba mimi ni bilionea Bill Gates.

Mimi kuandika kwamba mimi ni bilionea Bill Gates hakunifanyi niwe bilionea Bill Gates.

Thibitisha unachodai. Usiandike tu kama hadithi.
 
Last edited:
Back
Top Bottom