Unajua kinacholeta utata kwenye elimu hii ya unajimu ni kuhusianisha yanayotokea angani na maisha yetu hapa duniani. Hapo ndio kwenye tatizo.
Hata hivyo umeuliza swali sana. Ni hivii, sayari inapokua katika hali kama hiyo (Retrograde) huwa inakua haipo katika hali yake ya kawaida (direct motion). Hivyo inakua kama imeweka pause kwa kipindi chote inachokua retrograde.
Inakua kama vile mtu ambaye kaamua kujipa likizo kwa muda. Mfanyakazi anapojipa likizo ina maana anafunga ofisi. Ofisi inapofungwa ina maana hakuna huduma.
Hicho ndicho inachofanya Mercury, inapumzika kwa muda takribani siku 21 hadi 25. Inakua ina slow down. Na hufanya hivyo mara 3 had 4 ndani ya mwaka 1.
Utata mwingine kati ya sisi wanajimu na nyinyi upo hapa, kwamba wanajimu huamini kwamba Mercury ndio msimamizi wa masuala yote yanayohusu mawasiliano na masuala yote niliyotaja kwenye mada yangu.
Sasa kama msimamizi wa hayo mambo yupo likizo je nani atayasimamia hayo mambo?
Jibu lake inabidi sisi tusubiri mpaka muda ofisi itakapofunguliwa. Lini? Tarehe 19 august. Kwa hiyo mambo yote yanayosimamiwa na mercury inabidi yaachwe kwa sasa.
Unajua kwa nini mercury anasimamia hayo mambo?? Elimu hiyo naitoa darasani kwangu sio hapa.
Nimetumia lugha nyepesi kwa sababu ili hata asiyejua nae ajifunze.
Swali jingine tafadhali.