Unajisikiaje mara ghafla mke wako anavyoanza kuonekana mkubwa zaidi kuliko wewe?

Sijui kwann mimi sinaga hii mitizamo. Miminyf akonde labda ndio nitashtuka. Akininenepa au kufumuka hata sioni tabu. Acha tu aishi anavyotaka maisha haya sio kilankitu cha kukijali muda woote uko makini kama nurse wa zam shift ya usiku..Mwache ajiachie..avae anavyotka ale anavyotaka afanye anavyotaka.. kuna muda maisha hayakupi hii option.
 
Mambo ya kuachana na Mke miaka 2 ndio hayo sasa, utofauti uanzie angalau miaka 7 kwenda juu.
Ahahahah... what is wrong with the age??? Mimi sijawah kuona shida hata.

Yf mimi alinipiga kamba wakat tunaanza relationship 2010 kuwa na yeye pia kazaliwa 1989 kumbe baadae nikaja kugundua kazaliwa mwaka 1988. πŸ˜‚πŸ˜‚.

Bas unafikiri hata kuna shida naionaga kuhusu umri!? Walaaah!!. Age is just a number bwana. Tunaishi tu hata hatusumbuki na minor issues kama hizo. Kanizalia watoto wa4 na bado namuona yuko fiti tu
 
Manukato safi hata afike 50 utamuona kawaida ila kama humtunzi na hali za umaskini lazima awe kikongwe..

πŸ˜„πŸ˜„,
 
Ni matunzo tu..Wakati nchi zilizoendelea Wanawake wembamba ndio wanakimbiza soko la udangaji na kuolewa.huku bongo Mitukunyema yenye miswambwanda ETI ndo wanakimbiza Soko kiasi kwamba wanawake hawapati usingizi wanawaza kuongeza shape..!

Wengi hawajijali ni kusaka pesa na vicoba mwanzo mwisho..Gym inaonekana umalaya huku kwetu..Akishajifungua ndo kabisaa anajiona kashazeeka anaanza kujifunika na mavitenge na nguo za kushona..Hawazingatii Diet wala nini..Anaamka na mihogo analala na Ugali.mara chips kwa wingi hii yote ni mfumo wa maisha tuliyochagua

Kazi kwelikweli/ Job true true
 
Sasa si umweleze yeye sisi unatueleza itakusaidia wewe nini😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…