Unajisikiaje Single Mother anapompost mwanae kwenye mitandao?

Unajisikiaje Single Mother anapompost mwanae kwenye mitandao?

Vijana wa kizazi cha sasa mnachekesha kweli, Hivi single Maza anamapungufu gani?
Hebu tuona nafasi ya mwanamke katika mahusiano,
1. Kutimiza shida zako za kimwili na kukupa faraja(tendo la ndoa)
2.kuzaa na kulea watoto,
3. Ni mshauri na msiri wako
4.Mwangalizi wa nyumba /familia
5.msimamizi na mwangalizi wa miradi kama mnayo.
Je katika hayo lipi single Maza hawezi fanya mpaka mnawasema vibaya
Kukulinganisha wewe na alie zaa nae kila mara

Kwenda mbele na kurudi nyuma


Kama mtoto ana fanana na baba yake, kila akimuona anamkumbuka x wake

X wake alie zaa nae akitaka kumla anmla mtu


Mtoto kusalimiwa na bibi na babu wanne (uzao wa maajabu huo u unakuaga) yani bibi wa upande wa mme wake watamsalimia kama mjuu wao, na wazazi wa mme alie oa watamsalimia kama mjukuu wao
 
Habari zenu,

Hili ni swali kwa Vijana wabishi walioamua kuoa Single Mother.

Unajisikiaje pale unapoona Single Mother uliemuoa anampost mtoto wake na kuandika maneno kama My World, My Everything halafu Baba Mtoto nayeye anakuja kucomment My family.?

Kumbuka kuwa wewe hujawahi kutamkiwa hayo maneno na hata ukitamkiwa hauamini kuwa anamaanisha?

Aisee! Kweli mlioa Single Mother mna mioyo Migumu kulalaleki.
Tuache na wake zetu
 
Kuna mmoja alimanusura anikamate maana nilikuwa nshampenda sana, hela zake ananipa nimuwekee kuonesha ananiamin na kunikubali.

Shida ni mtoto walie zaa na x wake yupo kwa bibi mzaa baba,

Mimi naenda kumtembelea simu inaita kapiga bibi mzaa x, aongee weeee na bibi, kisha na mtoto, kisha na baba wa mtoto (utasikia baba fulani huyu hapa ongea nae).

Wakati akipewa simu ya kuongea na baba wa mtoto atajifanya ishara ya kunyari, basi watasalimiana hapo kwa sauti nzito nzito kisha anahamishia mada chap kuhusu mjadala wa mtoto wao na sijui karo, uniform ziwe nzuri, sijui aliumwa hawakumpa dozi ikaisha.

Wakimaliza bibi anasema kuna wifi yako pia msalimie,

Nikajisemea mateso yote haya ya nini? Hadi lini?

**** siku nikamtengenezea tukio la kumsapraizi usiku mnene kumtembelea kwake nikakuta hayupo na ilihal tulipokuwa tunachat alisema yupo home na analala.

Nilivyofika nikapiga simu haipokelewi, akaja kupokea baadae anasema nipp ndani ilihal nipo nje hajarudi.

Toka siku hiyo akili ikafunguka nikapata gear ya kutake off.
 
Back
Top Bottom