Unajisikiaje ukipewa DISLIKE kwenye comment yako?

Unajisikiaje ukipewa DISLIKE kwenye comment yako?

kwa kweli mi huwa najihoji mara 2 tatu why nipewe 👎

Kuna member kaibuka hapa yeye kila post abagawa Dislike tu sijui roho yake imekaaje kaaje humo ndani😅😅😅

Karibuni kwa Hoja na Love za kutosha mwenzenu nifurahi😍
Aahahaaaa
Screenshot_20230518-105637.png
Screenshot_20230518-105625.png
 
Kuna baadhi tunachukulia JF kama sehemu ya ku waste time lakini kuna wengine hii mitandao ya kijamii ndio maisha yao halisi.

Kuna mtu mwingine anakuwa hana thamani yeyote katika maisha yake kiasi kwamba akikaa bila kuingia mitandaoni hana interaction nyingine yeyote yenye tija katika maisha halisi.

Sasa basi watu wa hivi ili kujipa thamani, ndio utakuta wale wanaotukana watu bila sababu, kuna wale akiwashwa na mguu tu anaandika thread, kuna wale wa kulike kila comment, wa kucheka kila comment hata kama havichekeshi na kuna kama huyo jamaa kaja na mpya ya kudislike kila jambo. Nina yakini pasi na shaka jamaa hata hasomi comment, ana dislike tu kama vile awali alikuwa aki like tu; hii yote ili aongelewe tu.

Hakupata reception aliyodhamiria kwenye ku like sasa toka jana kaja kivingine kwa kudislike. Na kwa njia ya ajabu imepata muamko aliodhamiria maana limeongelewa (japo sitostaajabu ikiwa hizi thread za kulalamika hizo dislike zikawa zimetoka kwa huyo huyo anae dislike ili kuweka muamsho kwa kila anachokifanya kwa kutumia ID nyingine za kwake). Kuna waliokiri kabisa kuwa wanaanzisha thread na kuanza kujisifia wenyewe, kujitukana na kusuluhisha wenyewe kwa kutumia ID zao kadhaa.

Kuna mambo mawili, kwa yeyote anaeathirika na dislike kwenye comment yake basi hakika hana tofauti yeyote na huyo alie dislike, ni kwamba wote wanahitaji kutafakari mustakabali wa maisha yao, maana yanahuzunisha. Na kwa huyo anae dislike kila comment halkadhalika nae atafute japo hobby ya kupiga nyeto, inaweza ikampa faraja fulani kuliko kupoteza muda kwa dislike comment za kila mtu.
 
Back
Top Bottom