Kuna baadhi tunachukulia JF kama sehemu ya ku waste time lakini kuna wengine hii mitandao ya kijamii ndio maisha yao halisi.
Kuna mtu mwingine anakuwa hana thamani yeyote katika maisha yake kiasi kwamba akikaa bila kuingia mitandaoni hana interaction nyingine yeyote yenye tija.
Sasa basi watu wa hivi ili kujipa thamani, ndio utakuta wale wanaotukana watu bila sababu, kuna wale akiwashwa na mguu tu anaandika thread, kuna wale wa kulike kila comment, wa kucheka kila comment hata kama havichekeshi na kuna kama huyo jamaa kaja na mpya ya kudislike kila jambo. Nina yakini pasi na shaka jamaa hata hasomi comment, ana dislike tu kama vile awali alikuwa aki like tu.
Hakupata reception aliyodhamiria kwenye ku like sasa toka jana kaja kivingine kwa kudislike. Na kwa njia ya ajabu imepata muamko aliodhamiria maana limeongelewa (japo sitostaajabu ikiwa hizi thread za kulalamika hizo dislike zikawa zimetoka kwa huyo huyo anae dislike ili kuweka muamsho kwa kila anachokifanya).
Kuna mambo mawili, kwa yeyote anaeathirika na dislike kwenye comment yake basi hakika hana tofauti yeyote na huyo alie dislike, ni kwamba wote wanahitaji kutafakari mustakabali wa maisha yao, maana yanahuzunisha. Na kwa huyo anae dislike kila comment halkadhalika nae atafute japo hobby ya kupiga nyeto, inaweza ikampa faraja fulani kuliko kupoteza muda kwa dislike comment za kila mtu.