GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,645
- 10,867
Hata kama siyo wote , lakini wengi wataweza kuelewa wakiona mtuhumiwa ameamua kubadilika toka moyoni!
Fikiri, kwa mfano, alkijitokeza na kusema, "Ndugu Watanzania wenzangu, naomba mnisamehe! Nimetambua makosa yangu, na ninayajutia sana. Mnisamehe, na mnipe muda nirekebishe nilikoharibu"
Kwani kuna shida gani mtu kutoka hadharani na kuomba msamaha? Mbona hata kule "duniani" kuna watu wakubwa walishawahi kukosea, lakini walipotubu walisamehewa?
Nani anakumbuka kashfa ya Rais Bill Clinton na Monica Lewinsky? Naamini, kama Bill Clinton asingekubali kuwajibika kwa kuwaomba msamaha Wamarekani pamoja na mkewe, huenda angeondolewa Ikulu ya WHITE HOUSE kwa kashafa ya uzinzi.
Haina maana kuendelea kuficha makosa wakati uliotaka wasijue washajua kuwa wewe ndiye "mwizi". Bora ukubali na kuomba msamaha!
Ukiendelea kujitetea kwamba "hukulamba" sukari wakati "lips" za midomo yako ina mabaki ya sukari, utaishia kuonekana unajifanya una akili kuwazidi wanaokutuhumu kuwa umelamba sukari!
Kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu!
Watanzania ni waelewa na wapole pia! Wakiombwa msamaha hawatashupaza shingo!!!