Unajua kuna vijana walilala Miaka 309 bila kuamka?

Unajua kuna vijana walilala Miaka 309 bila kuamka?

Kila kitu cha Mwenyezi Mungu, sio sayansi tu
Nilikushangaa ulivyosema sayansi imekuja juzi. Wakati sayansi ni ya Mwenyezi Mungu. Kuanzia wewe ulivyo ni sayansi. Mvua inayonyesha ni sayansi. Jua ni sayansi, nyota, mwezi vyoote ni sayansi.
 
Qur'an inataja kisa cha vijana waliolala pangoni kwa muda mrefu kama mojawapo ya ishara za nguvu na hekima ya Allah. Hiki ni kisa cha "Watu wa Pangoni" (Ashabul Kahf), kilichoelezwa katika Surah Al-Kahf (18:9-26).

Maelezo ya Kisa:

1. Kukimbilia Pangoni:
Vijana hawa walikimbilia pangoni ili kuokoa imani yao wakati wa dhuluma kutoka kwa mtawala aliyewalazimisha waabudu masanamu. Waliomba msaada wa Allah na kulala humo.

Surah Al-Kahf (18:10):
"(Kumbuka) waliposema wale vijana, 'Mola wetu! Tupe rehema kutoka kwako, na utengeneze njia ya uongofu katika jambo letu.'”

2. Kulala kwa Miaka 309:
Vijana hao walilala kwa muda wa miaka 300 kulingana na kalenda ya jua, au miaka 309 kulingana na kalenda ya mwezi.

Surah Al-Kahf (18:25):
"Na wakakaa pangoni kwa miaka mia tatu, na wakaongezwa tisa."

3. Kuamshwa kwa Nia ya Kuonyesha Ishara ya Allah:
Baada ya muda huo mrefu, vijana hao waliamshwa, na kisa chao kilihifadhiwa kama ishara ya uwezo wa Allah wa kufufua waliokufa.

Surah Al-Kahf (18:19):
"Na tukawaamsha ili waulizane wao kwa wao. Mmoja wao akasema, 'Mmekaa hapa kwa muda gani?' Wakasema, 'Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.' Wakasema, 'Mola wenu anajua zaidi muda mliokaa...'”

4. Jinsi Walivyolindwa:
Allah alilinda miili yao kwa kuwafanya wageukegeuka kulala ili wasiharibike, na mlinzi wa nje wa pango alikuwa mbwa wao.

Surah Al-Kahf (18:18):
"Na ungalidhani kuwa wameamka, hali wao wamelala, na tunawageuza kulia na kushoto, na mbwa wao ameunyosha mkono wake kizingitini..."

Ujumbe na Mafunzo:

1. Kujitoa kwa Allah: Vijana hawa ni mfano wa watu wenye imani thabiti waliomtegemea Allah kwa kila hali.

2. Uwezo wa Allah: Inathibitisha kuwa Allah ana uwezo wa kufanya mambo yasiyowezekana kwa mtazamo wa kibinadamu, kama kulala kwa miaka mingi bila kuharibika.

3. Thamani ya Imani: Allah anawalinda wale wanaoshikamana na imani yao licha ya changamoto na dhuluma.

Kisa hiki ni ushuhuda wa imani na ishara ya nguvu ya Allah katika kulinda na kufufua viumbe vyake.
Hyo inaitwa CRYOSLEEP, ni aina ya kutunza mwili ambapo viungo vya ndani vya binadmu kuzima na kutunzwa kwenye baridi kwa muda unaotaka ukiwa umelala na kisha joto la mwili huanza kuja taratibu na ukiamka unakuwa hujaongezeka umri
 
Nani kafanyiwa hivi ? America wanafanya?
 
Nani kafanyiwa hivi ? America wanafanya?
Ukicheki aya ya 17 au 18 kama mas-hafu imeweka Bismllahi kama aya, inasema "Na unaliona jua linapopanda linapita mbali na pango" hyo ina maanisha walikuwa hawapati joto la jua hivyo kusababisha kuwa na hali ya baridi ndani ya pango
 
No no no. The BIG NO. Hiyo ni namna ya ujibuji wa maswali ya watu wasio na maarifa. Ni sawa na mtoto unamuuliza kwa nini umelamba sukari. Anajibu mbona na Athuman amelamba. Sasa wewe mzazi ulikuwa unataka kujua nani mwingine kalamba sukari au unataka kujua sababu za yeye kulamba sukari!!?

Jibu maswali kama mtu matured.

Halafu mimi ni miongoni mwa watu wanapinga kutumia lugha za kigeni katika kuingiza maarifa kwa watoto. Ila mifumo na utayari wa waAfrika uko mbali.
Matured. Hakuna kiswahili chake? Au ndio chawa wa wazungu?
 
4. Jinsi Walivyolindwa:
Allah alilinda miili yao kwa kuwafanya wageukegeuka kulala ili wasiharibike, na mlinzi wa nje wa pango alikuwa mbwa wao.

Surah Al-Kahf (18:18):
"Na ungalidhani kuwa wameamka, hali wao wamelala, na tunawageuza kulia na kushoto, na mbwa wao ameunyosha mkono wake kizingitini..."
Kwan kipindi icho mbwa walikua na uwezo wa kuishi miaka mingapi mkuu.
 
Matured. Hakuna kiswahili chake? Au ndio chawa wa wazungu?

Asalama leko allahu kibaruu
Muhammad lasuur.

Ningetaja maneno haya wala usingeongea hivyo, ewe mfuasi wa chombo/mpango cha kueneza tamaduni, mila na desturi za kiarabu (maana halisi ya uislam)
 
Hyo inaitwa CRYOSLEEP, ni aina ya kutunza mwili ambapo viungo vya ndani vya binadmu kuzima na kutunzwa kwenye baridi kwa muda unaotaka ukiwa umelala na kisha joto la mwili huanza kuja taratibu na ukiamka unakuwa hujaongezeka umri
Leo nilikuwa sijanywa CHAI asante sana
 
Asalama leko allahu kibaruu
Muhammad lasuur.

Ningetaja maneno haya wala usingeongea hivyo, ewe mfuasi wa chombo/mpango cha kueneza tamaduni, mila na desturi za kiarabu (maana halisi ya uislam)

tameer
Kwa akili yako. Nani ni chawa halisi wa wageni. Je ni wale ambao wanatamka maneno yaleyale ya lugha wageni mara 5 kwa siku. Au ni wale wengine ambao hutumia lugha ya kigeni kwa nasibu. Bila kuwa na mfumo maalum wa kutaja maneno hayo?
Ukijibu tafadhali, nakala iende kwa huyu Malaria 2
 
Back
Top Bottom