Unajua kwanini maji ya kuchemsha hupoteza ladha (flat taste)? Fahamu nini ufanye kurudisha ladha yake

Unajua kwanini maji ya kuchemsha hupoteza ladha (flat taste)? Fahamu nini ufanye kurudisha ladha yake

UNAJUA KWA NINI MAJI YA KUCHEMSHA HUPOTEZA LADHA?

Mbinu ya kuchemsha maji ni moja ya mbinu ya kuyafanya maji kuwa salama, kupitia mbinu hii utaweza kuua vijidudu, bacteria na virusi mbalimbali ambavyo vipo katika maji.

Ubaya wa njia hi ni kwamba, baada ya hapo maji yanakua hayana ladha (flat taste)

SABABU MAJI YA KUCHEMSHA KUKOSA RADHA

Unapo chemsha maji hewa ambayo huwa katika maji huondoka, na hewa iliyopo katika maji ndio hufanya maji kuwa na ladha.

UFANYE NINI KURUDISHA LADHA YA MAJI BAADA YA KUYACHEMSHA.

Ni rahisi sana, fanya hivi.

1. Yaache maji yapoe
2. Chukua vyombo viwili vitakavyotosha hayo maji
3. Uwe unayamimina kutoka chombo kimoja kwenda kingine Kama vile unayapooza, hakikisha unainua juu ili maji yawe yanashuka kwa kuporomoka.

Fanya Kama mara 10 hivi

Hii husaidia maji kuchanyikana na hewa tena na radha yake kurejea Kama kawaida.

Chukua hiyo
Asante sana mkuu yani asante sana
 
Me nimekuelewa mkuu asante nitajaribu, maana kunywa maji ya kuchemsha Ni kipengere unakua kama unakunywa dawa,
 
Haya maji wanakemia wanasema ni H20 ukichemsha hewa gani inatoka?
Na ukiyapoza ni hewa gani inachanganyika? Formular yake inakuwaje baada ya kuchemka na baada ya kupoza?

Wana kemia tusaidieni kwani ni kweli maji yanakuwa na radha tofauti baada ya kuyachemsha.




kuna mkemia atakuja hapa aseme hiyo radha inatoka kwenye vifaa au mazingira ulimochemshia.
[emoji2957]
 
Haya maji wanakemia wanasema ni H20 ukichemsha hewa gani inatoka?
Na ukiyapoza ni hewa gani inachanganyika? Formular yake inakuwaje baada ya kuchemka na baada ya kupoza?

Wana kemia tusaidieni kwani ni kweli maji yanakuwa na radha tofauti baada ya kuyachemsha.




kuna mkemia atakuja hapa aseme hiyo radha inatoka kwenye vifaa au mazingira ulimochemshia.
[emoji2957]
Scientific explanation

Boiling water removes dissolved oxygen and other gases.

The solubility of gases in liquids is decreased as temperature increases. This manifests as a problem when water is used for cooling, e.g. in a power plant.

The warm water returned to the river is depleted in oxygen, which can kill off the fish and other animals (crustaceans, molluscs, etc.)
 
Maji yana ladha kama vile mnavyosema **** tamu utamu wake upi
 
Hiyo gharama ya kuchemsha na huo mda wa kupoza, ni Bora ununue Lita 20 Kwa elfu 6 tu.
Mmmm!!! Hiyo 6000 kwa mtanzania mnyonge ni pesa ya kula simu nzima na familia nzima, akanunue maji ya kunywa??!!! Jamani maisha haya yaacheni tu
 
Akili ya kuambiwa changanya na yako.
Kuna walioambiwa wako uchumi wa Kati wakati JIJINI DAR watoto wanasomea chini ya miti huku wamekaa chini
Utapewa mfano wa Rashford alivyopigania wanafunzi wapewe chakula shuleni huko Uingereza. Uchumi ni taaluma za watu Na ndio maana hata A za uchumi ni Adimu. Haudiskasiki kirahisi rahisi
 
Kubana matumizi kwenye kununua maji ya elfu 6? Sasa ili uweze kujenga nyumba ya milioni 30 utatumia muda gani kuchemsha maji ili kuisave hiyo 30?

Matumizi hayabanwi kwa kula maharage au mchicha daily na ugali au kupiga mboga chukuchuku kwa kuhofia kununua nyanya za mia5 na kibaba cha mafuta cha 300.
Mungu akikujaalia nafuu ya Maisha usimalize maneno.
 
Mungu akikujaalia nafuu ya Maisha usimalize maneno.

Mkuu najua maisha yote ya kuanzia kula bata la hatari yaani msosi wa draft hadi kushindia chai asubuhi bila kitafunio ,mchana karanga za mia na usiku kipande cha jero cha tikiti,mimi nazungumzia kusave kwenye kununua dumu la maji Tsh 100 vs lita 18 ya elfu 6.
 
Kazi yoote ya Nini...Mimi SIONI Kama hayana ladha...nimeyazoea..

Ila nimeonja maji ya mvua...Yana ladha nzuri Sana..sikuweza TU kuyanwa
 
Back
Top Bottom