Unajua kwanini Wazungu wanapenda kusoma vitabu?

Unajua kwanini Wazungu wanapenda kusoma vitabu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Waafrika wanasoma vitabu, lakini Wazungu wana wasomaji wengi zaidi kuzidi Waafrika.

Kwa Wazungu, usomaji wa vitabu ni kama sehemu ya maisha ya wengi wao.

Unajua ni kwa nini? Naamini ni kwa sababu wamelelewa hivyo! Walijengewa hiyo tabia tokea wakiwa wadogo sana.

1. Wanaweza wasiwe wote, lakini nafahamu kuwa Wazungu wana kawaida ya kuwasomea watoto wao vitabu pindi wanapojiandaa kulala. Mtoto anapoingia kitandani kulala, mzazi huketi pembeni yake na kumsomea kitabu mpaka asinzie.

2. Wengine huanza kuwasomea watoto wao vitabu tokea wakiwa tumboni. Huamini kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuifinyanga tabia ya mtoto tokea akiwa tumboni mwa mamaye.

3. Nao wenyewe ni wasomaji. Ni rahisi mtoto kuiga kile anachokiona kwa wazazi wake. Watoto wa wasomaji huishia kuwa wasomaji.

Hizo ni baadhi ya mbinu wanazozitumia. Yeyote anaweza kuzitumia kuwajengea watoto wake tabia ya kujisomea vitabu vizuri.
 
photo_2024-04-08_01-38-03.jpg
 
Hivi tanganyika library kuna mahudhurio kweli
Maana wakati wetu tunasoma hizo sehemu ilikuwa laZima uende
Kujisomea vitabu mbalimbali
Badaye tena ilipokuja American library tukawa tunapavamia pia

Ova
 
Back
Top Bottom