Unajua kwanini Wazungu wanapenda kusoma vitabu?

Unajua kwanini Wazungu wanapenda kusoma vitabu?

Umejibu vema sana
1.vimeandikwa lugha Yao.
2.Bei ni rafiki kwa uchumi wao
Vitabu vya Kiswahili vipo vingi tu,

Majarida ya Kiswahili yapo mengi,

Fikiria hili,
Kule sekondari Kuna vitabu vya Kiswahili, vya riwaya
Katika darasa watoto wawili au watatu watasoma Ila wengine ambao Ni wengi wanakomaa na summary za mwalimu tu

Hapo unapata picha gani?
Kitabu ambacho kila mtu atasoma ni Ngoswe!

Kitabu Cha KUSADIKIKA Cha Shaaban Robert, ambacho hakina maudhui ya mapenzi, kinasomwa na wanafunzi wawili ambao wanaasili ya upenzi wa kusoma vitabu

Kuna haya majarida ya Fema, yanagawiwa mashuleni
Yanatoa Elimu mbalimbali za Makuzi, usafi, afya, maadili, mazingira, Uongozi n.k
Lakini hautakuta watoto wanachukua muda wao kusoma wapate Elimu,
Mara chache tu watasoma zile katuni Basi

Tabia ya kupenda kusoma ni janga kwetu,
Ni upumbavu kuanza kujitetea katika hili

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu bei nakubali 100%kwetu watu masikini sana tunahangaika na shillings za kula,kitabu elfu 30 anasa,Mimi Kuna kitabu kinauzwa 120k,Kila nikifikiria gharama najikuta naghairi,
Kitabu gani mkuu? Mimi vitabu vingi nanunua 10,000-15,000 tena najua huyu jamaa ananipiga. Ingawa hivi vitabu bei halisi si chini ya 100,000 ila wanafyatua copies mjini hapa.
 
Kitabu Cha Mzee Fulani anaitwa Arthur Maxwell
Kitabu gani mkuu? Mimi vitabu vingi nanunua 10,000-15,000 tena najua huyu jamaa ananipiga. Ingawa hivi vitabu bei halisi si chini ya 100,000 ila wanafyatua copies mjini hapa.
 
Hivi tanganyika library kuna mahudhurio kweli
Maana wakati wetu tunasoma hizo sehemu ilikuwa laZima uende
Kujisomea vitabu mbalimbali
Badaye tena ilipokuja American library tukawa tunapavamia pia

Ova
Kule kuna free wifi na mtv wa kwenda
 
# roca fella

Hata mimi ni msomaji kiasi wa vitabu pale ninapo pata nafasi huwa ninafurahia tukio hilo kwa maana kusoma ni kuongeza maarifa na kupata mwangaza.
Vinzur San, vp huyo Kwa picha ndio wew🤒😋
 
Sababu vimeandikwa lugha yao ya nyumbani, wewe unataka kuniambia Watoto wa Mama Ntilie haukukisoma? Machozi Jasho na Damu haukukisoma? Rais anamtaka Mke wangu haukukisoma? Vingeandikwa kigriki ungesoma?
Sidhani kama lugha ndiyo tatizo. Vitabu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ni vingi sana nchini lakini wasomaji ni wachache mno ukilinganisha na mataifa mengine.

Hata wasomi wengi wa Tz huwa wakishatunukiwa shahada zao hupeana talaka na vitabu. Ni tofauti na kwa "wenzetu", wao wamefanya urafiki na vitabu.
 
Bei Jing ngapi?
 
Mama yake Dr Carson aliwapa hii task Dr Carson na ndugu yake. Imagine huyo mama alikuwa hajui kusoma.
Mkuu unaona sasa what came out of that task...

Vitabu ni muhimu sana.... Nimekuwa msomaji sana siku za karibuni duuh sijui nilikuwa wapi siku zote, my life is changing for the better hata hapa nipo na kitabu changu nasoma.
 
Back
Top Bottom