Vitabu vya Kiswahili vipo vingi tu,
Majarida ya Kiswahili yapo mengi,
Fikiria hili,
Kule sekondari Kuna vitabu vya Kiswahili, vya riwaya
Katika darasa watoto wawili au watatu watasoma Ila wengine ambao Ni wengi wanakomaa na summary za mwalimu tu
Hapo unapata picha gani?
Kitabu ambacho kila mtu atasoma ni Ngoswe!
Kitabu Cha KUSADIKIKA Cha Shaaban Robert, ambacho hakina maudhui ya mapenzi, kinasomwa na wanafunzi wawili ambao wanaasili ya upenzi wa kusoma vitabu
Kuna haya majarida ya Fema, yanagawiwa mashuleni
Yanatoa Elimu mbalimbali za Makuzi, usafi, afya, maadili, mazingira, Uongozi n.k
Lakini hautakuta watoto wanachukua muda wao kusoma wapate Elimu,
Mara chache tu watasoma zile katuni Basi
Tabia ya kupenda kusoma ni janga kwetu,
Ni upumbavu kuanza kujitetea katika hili
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app