Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Mkuu
Unajua kuwa unazidi kuthibisha madai yangu kwamba imani hizi zinasababishwa na uvivu wa kufikiri?

Daktari akishindwa kutibu ugonjwa tunakimbilia kusema ni uchawi au majini bila ya kujishughulisha kutafuta kujua tatizo ni nini ambapo inawezekana linaelezeka kibaiologia katika namna ambayo sisi hatujaielewa bado.

Umesema sayansi imeshindwa kutoa majibu kuhusu chanzo cha uhai. Ni kweli ,sayansi haijaelezea kila kitu lakini kwa nini hiyo isiwe chachu ya sisi kushughulisha akili zetu kufanya uchunguzi ili tupate majibu mazuri zaidi yasiyo na utata na yanayothibitishika na badala yake tunajitungia majibu mepesi yasiyothibitishika na yenye utata?

Unasema sayansi imeshindwa kuelezea laana, maisha baada ya kifo mikosi n.k

kwanza kabisa sayansi sio tu imeshindwa kuvielezea, hata haijathibitisha kama vipo. Ni dhana za kifikirika zaidi hivyo haviwezi kuthibitishika hivyo haziwezi kuelezeka.
 
Reactions: Tsh
Unajua hivyo au unaamini?
 
Hapa sijaelewa hoja yako ni ipi.
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza; na tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema walio kufuru, Hizi si chochote ila hadithi za watu wa kale.
 
God loves you. He doesnt judge you. He know you are blind because you have believed into the thoughts of the imagination which is of your father the devil.
If human beings would stop listening to the thoughts they would all become free. Everything starts with a thought.
 
Unajua hivyo au unaamini?
Na lau ungeli ona watavyo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akawaambia: Je, si kweli haya? Na wao watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu ni kweli. Yeye atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyo kuwa mnakataa.
 
“Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.”
— Warumi 1:28 (Biblia Takatifu)


Yaan fahamu zako zilivyogoma kumtambua haimpunguzii chochote Mungu ktk Milele yake, haupunguzi UTUKUFU WAKE WALA UKUU WAKE...sana anakuacha ufuate akili zako zisizofaa uendelee kuyafanya yasiyopasa..
hiyo siku mbele zake ktk hukumu ndio utajua hujui..
 
Acha kujificha kwenye maneno yasiyo na msingi. Unataka kujua kuhusu mwanzo wa kutajwa mungu lazima uwe specific mungu yupi, babu zako walitaja mizimu kabla hawajetewa biblia na quran.
Kuna mungu wa dini zaidi ya 4000 wenye historia tofauti kulingana na asili ya binadamu husika.
 
Kwanini ni lazima kuamini na sio kujua?
 
Ww ni mjinga wa tafsiri ya neno imani, Imani sio uhalisia. Ishia tu hapo hapo usiendelee.
 
Unanihubiria badala ya kutoa hoja.
Toa hoja
 
ushuhuda kidogo tafadhali ilikutokea nini..
 
Kwanini ni lazima kuamini na sio kujua?
akika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba.
 
akika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba.
Mkuu hujui maana ya mjadala.
Hakuna hoja unayoileta Bali maneno matupu tu.
Hatuwezi kujadiliana.
 
Kwani laana mikosi mabalaa hayapo kwenye jamii.
Ujawahi sikia daktari anasema tumepima KILA kitu na hatuoni ugonjwa?
 
Mkuu hujui maana ya mjadala.
Hakuna hoja unayoileta Bali maneno matupu tu.
Hatuwezi kujadiliana.
Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu. Na hapana wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na bila ya shaka zimekujia baadhi ya khabari za Mitume hao.
 
Mkuu hujui maana ya mjadala.
Hakuna hoja unayoileta Bali maneno matupu tu.
Hatuwezi kujadiliana.
Nakuchapa kwa aya tuu!

Bado kofi lenye maelekezo ya kashifa juu ya mola wako! Wewe si unajua tukana mamba angali kuvuka mto bado, Na usubiri habari yako baladhuri mjaa laana wewe!
 
Kwani laana mikosi mabalaa hayapo kwenye jamii.
Ujawahi sikia daktari anasema tumepima KILA kitu na hatuoni ugonjwa?
Sawa tuanze taratibu.
Laana ni nini?
Mabalaa yapi unayazungumzia?

Kwanini vipimo vya daktari kutoona ugonjwa kufanye ugonjwa huo uwe wa kichawi?

Unatambua kuwa yanaweza kuibuka magonjwa mapya ambayo hatujayajua kabla?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…