Cornwallis
JF-Expert Member
- Oct 30, 2022
- 940
- 853
- Thread starter
- #261
MkuuKuna aina mbili za magonjwa moja ya kibailogia na magonjwa ya kiroho.Yote matokeo yake uonekana kimwili.
Upo ukimwi,kansa,ukoma nk yapo ya kutengenezwa haya mtu anapona kabisa kupitia tiba za kiroho na sio kwa tiba za kisayansi. Hata madaktari wa hospital wanajua kuhusu hili thus wao wakishindwa kwa vipimo na utaalamu wao wote wanakushauri hili sio la kidaktari jaribu tiba za kiroho.
Hakuna uthibisho kwamba dini inasema jua linazunguka duniani.
Mfano sayansi haiwezi kujibu KWA usahihi kuhusu viumbe visivyoenekana mfano UFO, majini, malaika.
Sayansi imeshindwa kutupa majibu kuhusu asili ya uhai, majibu kuhusu muunganiko wa ROHO, nafsi na mwili, kuhusu maisha baada ya kifo, ndoto, laana na mikosi kwa uchache tu hivi.
Unajua kuwa unazidi kuthibisha madai yangu kwamba imani hizi zinasababishwa na uvivu wa kufikiri?
Daktari akishindwa kutibu ugonjwa tunakimbilia kusema ni uchawi au majini bila ya kujishughulisha kutafuta kujua tatizo ni nini ambapo inawezekana linaelezeka kibaiologia katika namna ambayo sisi hatujaielewa bado.
Umesema sayansi imeshindwa kutoa majibu kuhusu chanzo cha uhai. Ni kweli ,sayansi haijaelezea kila kitu lakini kwa nini hiyo isiwe chachu ya sisi kushughulisha akili zetu kufanya uchunguzi ili tupate majibu mazuri zaidi yasiyo na utata na yanayothibitishika na badala yake tunajitungia majibu mepesi yasiyothibitishika na yenye utata?
Unasema sayansi imeshindwa kuelezea laana, maisha baada ya kifo mikosi n.k
kwanza kabisa sayansi sio tu imeshindwa kuvielezea, hata haijathibitisha kama vipo. Ni dhana za kifikirika zaidi hivyo haviwezi kuthibitishika hivyo haziwezi kuelezeka.