Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Mkuu hujathibisha chochote kati hivyo nilivyokuomba uthibitisho.
 
Falsafa (arm chair thinking) ikiingia sana kichwani, huwa inampelekea mtu kuona kuwa vilivyopo vyote havipo, halafu vile ambavyo havipo, ndiyo vinaonekana kuwa vipo
Unaweza kutaja vitu ambavyo falsafa inamfanya MTU aone havipo na vile ambavyo havipo vionekane kuwepo?
 
Mzimu una nguvu kwako na sio kwa wote.
Mungu ni jina na ndani ya jina ipo nguvu
Kwa nini unadhani jina Mungu ndio lenye nguvu na sio mzimu?

Aliyekwambia na kukuaminisha jina Mungu ndio lenye nguvu ni nani?

Bila shaka ni dini..Ndio maana huwa nasema waafrika mlisha haribiwa na dini.

Unge aminishwa na kuambiwa hiyo nguvu inaitwa jina Mzimu tangu utotoni mwako unge amini mzimu ni jina lenye nguvu.

Kwa hiyo nahitimisha kwamba una mwamini Mungu kwa HOFU za kidini kwamba usipo amini uwepo wake mwisho wa siku utachomwa Moto..

Amka mwafrika.....[emoji1][emoji1]
 
Tatizo lenu waumini.. mkiulizwa maswali yenye hoja nzuri.. mnakimbilia vitisho vitisho.

Hizi zama za werevu sio za wajinga wajinga.. jifunzeni kujibu maswali yenye hoja , kwa hoja nzuri ya jibu.. sio vitisho vitisho vya mwaka 47
Umechukuliwa msukule wewe
 
Hivyo unaamini kwa kuogopa kuitwa mpumbavu? Kama yupo kwanini aniache niwe mpumbavu na mwingine awe mwelewa? Unaweza kuthibitisha kuwa yupo?
Ni rahisi kuthibitisha yupo badala ya kuthibitisha kuwa hayupo. Pole kwa kusema mpumbavu, nimenukuu tu biblia.
 
Wewe mwanadamu uliye mtengeneza Mungu umekujaje duniani? (Binadamu wa kwanza kajaje?)
 
Wewe mwanadamu uliye mtengeneza Mungu umekujaje duniani? (Binadamu wa kwanza kajaje?)
Sijui alikujaje....hill halifanyi jibu liwe mungu kaumba..

Inabifi tusiwe wavivu wa kufikiri ,tutulize akili na tufanye uchunguzi tupate majibu yenye mantiki zaidi na sio kujitungia majibu ya harakaharaka yasiyothibitishika.
 
Hizi hoja ni ngumu na hakuna wa kukupa Majibu kwa wakati huu sana utaishia kushambuliwa tu na wanaoamini katika nadharia hii.

Nenda katafute kitabu kinachoitwa HOMA YA DUNIA ni ngumu kukipata ila kinapatikana. Hakika ukikisoma utaona namna ambavyo Dunia imebadilishwa na Mfalme Constantine kiasi hivi sasa huwezi pata ukweli wowote kumuhusu Mwenyezi Mungu.

Ni huzuni kwa upande wangu kuona Mungu muweza wa yote Bado amekaa kimya. Hata baada ya kupotezewa viumbe wake kiasi hata kuandaa Jeshi la malaika ili siku Moja waje waiangamize na kutoka hukumu kwa Dunia hii aliyoitengeneza kwa uweza wake mwenyewe kwa kile kinachosemekana kumuhasi na kutotii kile anachokitaka Mwanadamu wake awe.
 
Hayupo, angekuwepo asingejificha tumtafute na tutakaomkosa atuchome moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…